TETESI ZA USAJILI ULAYA ZILIZO TAMBA LEO….
Matumaini ya Arsenal kumsajili
Jackson Martinez, 28, kutoka Porto yamekwisha baada ya mchezaji huyo
kutoka Colombia kusaini mkataba wa miaka minne Atletico Madrid (AS).
Manchester United wanamtaka
Sergio Ramos ili kubadilishana na David De Gea. Real Madrid wanamtaka De
Gea, 24, pamoja na pauni milioni 20 za kumnunua Ramos. Utd watamzuia De
Gea kuondoka iwapo Real watakataa mpango huo (Daily Star).
West Ham hawatomuuza Andy Carroll msimu huu (Sun).
Newcastle wapo katika nafasi
kubwa ya kumsajili Charlie Austin, 25 kwa pauni milioni 14. Mchezaji
huyo anatakiwa na Southampton, Chelsea na West Ham (Daily Express)
Newcastle na Stoke wanamtaka
winga kutoka Ukraine Yevhen Konoplyanka ambaye atakuwa mchezaji huru
baada ya mkataba wake kukamilika na Dnipro (Daily Mirror).
Stoke City wanatarajia dau la
pauni milioni 8 kutoka Chelsea kumchukua kipa Asmir Begovic, 28, na
watataka Victor Moses kuunganishwa katika mkataba huo (Daily Telegraph).
Hata hivyo matumaini ya Chelsea
yana wasiwasi baada ya Moses, 24, kusema hana uhakika kama anataka
kurejea Stoke alipocheza kwa mkopo msimu uliopita Times).
West Brom wanajiandaa kumfanya Demba Ba, 30, mchezaji anayelipwa zaidi (Birmingham Mail)
West Ham wamekubali mkataba wa pauni milioni 12 kumsajili kiungo wa Marseille Dimitri Payet, 28 (Daily Mail).
Rais wa zamani wa Real Madrid,
Ramon Calderon amesema Manchester United watakuwa na “bahati sana”
kumsajili Sergio Ramos, 29 (TalkSport).
Meneja wa Tottenham Mauricio
Pochettino ana matumaini ya kuwashawishi wachezaji wake muhimu, kwa
kumfaya kipa Hugo Lloris, 28, kuwa nahodha na Harry Kane, 21, kuwa naibu
nahodha (Daily Mirror).
Winga wa Chelsea Mohamed Salah,
23, anatarajiwa kuwaambia Fiorentina kama atasalia Italia au la, baada
ya kuichezea klabu hiyo kwa mkopo msimu uliopita (Daily Telegraph).
Sunderland wametoa dau la zaidi
ya pauni milioni 11 kumchukua kiungo wa PSV Eindhoven Georginio
Wijnaldum, 24, ambaye anasakwa pia na Newcastle (Guardian).
Manchester United wameacha
kumfuatilia Ilkay Gundogan ambaye huenda akasalia Borussia Dortmund
wakati Utd wakitafuta kuingo kwingineko (Daily Star)
Uhamisho uliothibitishwa nitakujulisha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni