THIERRY HENRY-ALEXIS SANCHEZ ATAIPA UBINGWA ARSENAL... WAKIONGEZA WAPYA!!!!!!!
Wachezaji wanaohusishwa na kutua Arsenal ni pamoja na Fowadi wa FC
Porto, Jackson Martinez, Kiungo wa AS Monaco Geoffrey Kondogbia,
Mchezaji wa Borussia Dortmund Sven Bender na Kiungo toka Southampton,
Morgan Schneiderlin.
Akiongelea kuhusu hali ya Arsenal, Thierry Henry, ambae ndie
anashikilia Rekodi ya Ufungaji Bora ya Arsenal na alikuwa Mchezaji wa
kile Kikosi cha Timu hiyo cha 2003/04 ambacho hakikufungwa kwenye Ligi
Msimu mzima, amesema: "Kama shabiki wa Arsenal, naungoja kwa hamu Msimu
ujao na natarajia tutaleta wapya, Wachezaji wapya lakini kama unae mtu
kama Alexis Sanchez, lolote linaweza kutokea. Anaweza kutupa Ubingwa!"
Aliongeza: "Tizama alivyofanya kwenye Fainali ya FA CUP na nini amekuwa akifanya tangu aje hapa. Amekuwa ni hatari! "
Katika Msimu wake wa kwanza na Arsenal, Sanchez alifunga Bao 24.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni