INTERNATIONAL CHAMPIONS CUP: MAN UNITED YASHINDA, DEPAY AFUNGUA AKAUNTI, SASA BARCA JUMAMOSI!
Hadi Mapumziko, Man United walikuwa mbele kwa Bao 2-1 kwa Bao za
Juan Mata na Depay na San Jose Earthquakes kufunga Bao lao kupitia
Alashe.
Bao la 3 Man United lilifungwa na Chipukizi wao kutoka Brazil Andreas Pereira.
+++++++++++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Manchester Uniteed 3
-Juan Mata Dakika ya 32
-Memphis Depay, 37,
-Andreas Pereira, 61
San Jose Earthquakes 1
-Fatai Alashe Dakika ya 42
+++++++++++++++++++++++++++++
Kama ilivyokuwa katika mechi yao ya kwanza ambayo waliifunga Klabu
ya Mexico, Club America, 1-0, Meneja wa Man United, Louis van Gaal,
alibadili Wachezaji karibu wote wa Man United kwa ajili ya Kipindi cha
Pili na kuwaingiza Jesse Lingard, Jony Evans, Chris Smalling, Ander
Herrera, Adnan Januzaj, Bastian Scheinsteiger, Tyler Blackett, Paddy
McNair na Andreas Pereira.
Mechi inayofuata kwa Man United Jumamosi Usiku katika Mashindano haya ya International Champions Cup.
VIKOSI VILIVYOANZA:
San Jose (4-2-3-1): Bingham; Wynne, Bernardez, Goodson, Stewart; Pierazzi, Alashe; Cato, Garcia, Salinas; Amarikwa.
Man United (4-2-3-1): Johnstone; Darmian, Jones, Blind, Shaw; Schneiderlin, Carrick; Mata, Depay, Young; Rooney.
REFA: J. Guzmán
MECHI ZA MAN UNITED:
-ZIARA USA
Ratiba/Matokeo:
18 Jul: Man United 1 Club America 0
22 Jul: Man United 3 San Jose Earthquakes 1
25 Jul: FC Barcelona [Saa 5 Dak 10 Usiku]
30 Jul: Paris Saint-Germain [Saa 10 Dak 10 Alfajiri]
LIGI KUU ENGLAND
Agosti 8 [Saa 1445]: Tottenham Hotspur [Old Trafford]
Agosti 14 [Saa 2145]: Aston Villa [Villa Park]
UCL
Agosti 18/19 [Saa 2145]: UEFA Championz Ligi-Mechi ya Kwanza Raundi ya Mchujo
LIGI KUU ENGLAND
Agosti 22 [Saa 1445]: Newcastle United [Old Trafford]
UCL
Agosti 25/26 [Saa 2145]: UEFA Championz Ligi-Mechi ya Marudiano Raundi ya Mchujo
LIGI KUU ENGLAND
Agosti 30 [Saa 1800]: Swansea City [Liberty Stadium]
LVG ADOKEZA STRAIKA MPYA KUTUA, MAN UNITED KUIVAA SAN JOSE EARTHQUAKES!
Man United imehusishwa na Mastraika wenye Majina makubwa katika
kipindi hiki cha Uhamisho kinachokwisha Septemba Mosi lakini wote hao
sio huyo 'Straika wa Siri' kwa kauli ya Van Gaal.
Wiki hii, Van Gaal alitoboa kuwa Kepteni wake, Wayne Rooney, ndie
atatumiwa kama Straika mkuu licha ya Msimu uliopita kumtumia kama Kiungo
katika Mechi nyingi.
Baada ya Robin van Persie kuuzwa kwa Fenerbahce ya Uturuki na
kutokubadili Mkataba wa Radamel Falcao kutoka wa Mkopo kwenda wa kudumu,
Man United imebaki na Mastraika Watatu tu wanaotambulika, Rooney,
Javier Hernandez 'Chicharito' na Kijana James Wilson.
Huku wakihusishwa na Mastraika wakubwa, Van Gaal, akiongea kabla ya
Mechi yao ya Jumatano Asubuhi huko Avaya Stadium Mjini San Jose,
California, alieleza: "Sio Straika ambae Wanahabari wanamtaja. Lakini
itabidi mngoje. Uhamisho mwisho ni Septemba 1!"
Miongoni mwa Mastraika ambao Man United wamehusishwa kutaka
kuwanunua ni pamoja na Edinson Cavani, Robert Lewandowski, Karim
Benzema, Harry Kane, Thomas Muller, Gonzalo Higuain, Gareth Bale na
Cristiano Ronaldo.
MECHI ZA MAN UNITED:
-ZIARA USA:
18 Julai: Club America [Man United imeshinda 1-0, Morgan Schneiderlin]
22 Julai: San Jose Earthquakes [Saa 12 Dak 10 Asubuhi]
25 Julai: FC Barcelona [Saa 5 Dak 10 Usiku]
30 Julai: Paris Saint-Germain [Saa 10 Dak 10 Alfajiri]
LIGI KUU ENGLAND
Agosti 8 [Saa 1445]: Tottenham Hotspur [Old Trafford]
Agosti 14 [Saa 2145]: Aston Villa [Villa Park]
UCL
Agosti 18/19 [Saa 2145]: UEFA Championz Ligi-Mechi ya Kwanza Raundi ya Mchujo
LIGI KUU ENGLAND
Agosti 22 [Saa 1445]: Newcastle United [Old Trafford]
UCL
Agosti 25/26 [Saa 2145]: UEFA Championz Ligi-Mechi ya Marudiano Raundi ya Mchujo
LIGI KUU ENGLAND
Agosti 30 [Saa 1800]: Swansea City [Liberty Stadium]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni