tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

23 Julai 2015

INTERNATIONAL CHAMPIONS CUP: SUAREZ AISAIDIA BARCA KUIPIGA LA GALAXY!


BARCA-ULAYA15Wakicheza huko Rose Bowl, Pasadena, California, Mabingwa wa Spain na Ulaya, FC Barcelona wameifunga Timu ya Marekani LA Gallaxy Bao 2-1 kwenye Mechi ya International Champions Cup.
Bao za Barcelona zilifungwa na Luis Suarez, Dakika ya 45, na Sergi Roberto, Dakika ya 56, wakati LA Galaxy walifunga Bao lao Dakika ya 90 kupitia Tommy Meyer.
Hii ni Mechi ya kwanza ya Barcelona tangu watwae Ubingwa wa Ulaya Mwezi Mei walipoifunga Juventus 3-1 lakini Kocha wao, Luis Enrique, alicchagua Kikosi imara ingawa kilikuwa na Wachezaji Watatu tu waliocheza Fainali hiyo ya Ulaya ambao ni Suarez, Sergio Busquets na Ivan Rakitic.
VIKOSI:
LA GALAXY (Mfumo 4-4-1-1): Rowe; Gargan, DeLaGarza, Leonardo, Dunivant; Husidic, Walker, Juninho, Maganto; Gerrard; Keane.
Akiba: Buddle, Vayrynen, Meyer, Lassiter, Lletget, Garcia, Wolverton, Romney, Jamieson, Steres, Mendiola, Villarreal, McBean, Sorto, Rogers.
BARCELONA (Mfumo 4-3-3): Masip; Douglas, Mathieu, Bartra, Adriano; Sergi Roberto, Busquets, Rakitic; Pedro, Suarez, Rafinha.
Akiba: Munir, Sergi Samper, Vermaelen, Sandro Ramirez, Halilovic, Gumbau, Jordi Alba, Jose Suarez, Pique, Iniesta, Ter Stegen.
REFA: Ismail Elfath

Hakuna maoni: