'MESSI NI PELE WA KIZAZI HIKI!'
Pele, Lejendari wa Brazil ambae Jina lake kamili ni Edson Arantes
do Nascimento, ndie anaesifika kuwa Mchezaji Bora kabisa katika
Historia ya Soka kwa kuiwezesha Brazil kutwaa Kombe la Dunia maraa 3.
Messi, mwenye Miaka 28, alififia mwanzoni mwa Msimu uliopita lakini
akalipuka baadae na kuibeba Barcelona kutwaa Trebo, yaani Ubingwa wa La
Liga, Copa del Rey na UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Hata hivyo, Messi amepondwa Nchini kwao Argentina baada ya kushindwa kutwaa Copa America walipobwagwa na Chile kwenye Fainali.
Belletti, Raia wa Brazil ambae alitwaa Ubingwa wa La Ligas mara 2
na UEFA CHAMPIONZ LIGI mara moja akicheza na Messi huko Barcelona,
anaamini Messi hana mfano katika kizazi hiki na hastahili kuzomewa huko
kwao Argentina.
"Messi ndio Pele wa kizazi hiki," Amenena Belleti, "Sielewi kwanini
kwao wanamponda. Huwezi kumponda Mchezaji kama Messi. Lakini hii pia
ilitokea kwa Ronaldinho huko Brazil. "
Belletti pia alimtetea Mbrazil mwenzake Neymar ambae alitolewa kwa
Kadi Nyekundu kwenye Copa America na kisha kufungiwa Mechi 4 na kuzikosa
Mechi za Brazil ambayo ilikuja kutolewa Robo Fainali.
Kuhusu Neymar, Belletti amesema: "Bado ni Kijana. Watu wanadhani ana Umri mkubwa. Bado ana muda wa kukomaa."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni