RAHEEM STERLING AIFUNGIA CITY MECHI YAKE YA KWANZA!
Katika Mechi ya Mashindano ya International Champions Cup, City ilishinda kwa Penati 5-4 na Ijumaa huko Australia.
Bao hlo la Sterling, ambae alinunuliwa kwa kitita cha Rekodi ya Uingereza cha Pauni Milioni 49 hapo Julai 14 kutoka Liverpool, lilidumu hadi Dakika ya 8 tu pale Miralem Pjanic alipofumua shuti la mbali na gemu kuwa 2-2.
City walikwenda 2-1 kwa Bao la Dakika ya 57 la Kelechi Iheanacho na AS Roma kuipeleka Gemu kwenye mikwaju ya Penati 5 waliposawazisha Dakika ya 87 kwa Frikiki ya Adem Ljajic.
Katika Penati hizo, Kipa wa City Joe Hart aliokoa Penati 2 na kufunga Penati ya mwisho ya ushindi.
VIKOSI VILIVYOANZA:
AS ROMA: Sanctis, Torosidis, Manolas, Romagnoli, Pjanic, Ucan, Florenzi, Gervinho, Iturbe, Totti
MAN CITY: Caballero, Sagna, Kompany, Clichy, Mangala, Sterling, Manuel Garcia, Fernando, Zucullini, David Silva, Iheanacho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni