tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

24 Julai 2015

RIPOTI-MAN UNITED, PSG ZAAFIKI DI MARIA, ADA £45M NA USHEI!

DimariaManchester United na Paris Saint-Germain zimefikia makubaliano juu ya Uhamisho wa Angel Di Maria kwa mujibu wa Ripoti kutoka huko France.
Ripoti hizo zimedai PSG imetoa Ofa ya Pauni Milioni 45 kumnunua Staa huyo wa Argentina kutaka Man United na Dau hilo lina nyongeza ya Bonasi zitakazotokana na mafanikio yake akiwa na PSG.
Kwa mujibu wa Jarida la kuaminika la France Football Ofa hiyo ya PSG imekubaliwa na Man United na kilichobaki ni Mchezaji mwenyewe kukubaliana Maslahi yake binafsi.
Inaaminika PSG iko tayari kumpa Di Maria, mwenye Miaka 27, Mkataba wa Miaka Mitano utakaomlipa Pauni 134,000 kwa Wiki.
Di Maria alijiunga na Man United kutoka Real Madrid mwanzoni mwa Msimu uliopita kwa Dau la Rekodi ya Uingerezan la Pauni Milioni 59.7 lakini baada ya kuanza vizuri huko Old Trafford akapoteza mwelekeo na kuanza kusuasua.
Zipo dalili kuuzwa kwa Di Maria kutafungua njia kwa ununuzi wa Straika badala yake kwa vile tayri Man United wanae Winga mbadala wake ambae ni Memphis Depay alienunuliwa kutoka PSV Eindhoven.
Depay aliibeba PSV kutwaa Ubingwa huko Uholanzi na yeye kuibuka kuwa ndie Mfungaji Bora wa Ligi ya huko kwao.
 

Hakuna maoni: