tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

24 Julai 2015

KIPONDO CHA RED BULLS-MOURINHO AMTETEA KIPA MPYA 'MCHOVU'!!

ASMIR-BEGOVICMENEJA wa Chelsea Jose Mourinho amemtetea Kipa 'mchovu' Asmir Begovic ambae mapema Leo akidakia kwa mara ya kwanza alitunguliwa Bao 4-2 na New York Red Bulls.
Begovic, Raia wa Bosnia mwenye Miaka 28, aliingizwa Kipindi cha Pili kumbadili Thibaut Courtois katika Mechi hiyo iliyochezwa Georgia Dome huko Georgia, USA.
Mara baada ya kipondo hicho, Mourinho alisema: "Hata tungeshinda 10-1 nisingefurahia. Begovic hakuwa shapu kwa sababu ya uchovu wa mazoezi. Katika Gemu ijayo na PSG ataanza."
Mechi hii na New York Red Bulls ni ya kwanza kwa Chelsea ambayo itacheza Mechi 3 Ziarana USA.
Wakiwa Chelsea wanaongoza 1-0 kwa Bao la Loic Reimy, Mourinho alimpumzisha Thibaut Courtois wakati wa Haftaimu na kumuingiza Begovic, waliemnunua toka Stoke City mapema Mwezi huu, lakini akawa chekeche na kuruhusu bao 4 za Red Bulls moja likifungwa na Kinda wa Mika 16 Tyler Adams.
Mourinho ameeleza: "Nilishangazwa na udhaifu wetu. Nilishangazwa hatukuwa wazuri Kipindi cha Pili kukabiliana na yale."
Jumamosi Chelsea watacheza na Mabingwa wa France Paris St-Germain huko North Carolina na kisha kuwavaa Mabingwa wa Spain na Ulaya, FC Barcelona huko Washington DC hapo Julai 29.
Agosti 2 Chelsea itarudi Jijini London na kutinga Wembley Stadium kucheza Mechi ya kufungua pazia Msimu mpya ya kugombea Ngao ya Jamii dhidi ya Mabingwa wa FA CUP Arsenal.
Chelsea wataanza utetezi wao wa Ubingwa wa Ligi Kuu England hapo Agosti 8 kwa kucheza na Swansea City Uwanjani Stamford Bridge.
VIKOSI VYA CHELSEA v NEW YORK RED BULLS:
KIPINDI CHA KWANZA: Courtois, Ivanovic (capt), Cahill, Zouma, Azpilicueta, Fabregas, Mikel, Traore, Oscar, Moses, Remy.
KIPINDI CHA PILI: Begovic, Aina (Solanke 71), Zouma, Terry (capt) Azpilicueta, Ramires, Matic, Hazard, Loftus-Cheek, Oscar, Diego Costa.
AKIBA HAWAKUTUMIKA: Chalobah, Clarke-Salter.

Hakuna maoni: