WAYNE ROONEY KURUDI KUICHEZEA EVERTON!
Rooney, mwenye Miaka 29, ataichezea Everton Mechi hiyo hapo Agosti 2 dhidi ya Villarreal huko Goodison Park Jijini Liverpoool.
Baada ya kuihama Everton Mwaka 2004 na kwenda Man United, Rooney,
alieanzia Soka lake la utotoni kwenye Chuo cha Everton, amekuwa
hakaribishwi vyema Goodison Park na Mashabiki wa Timu hiyo na Mwaka 2008
aliamsha hasira kubwa aliporudi Goodison Park kucheza dhidi ya Everton
na kuonekana akibusu Beji ya Man United.
Akikaririwa kwenye Tovuti ya Everton, Rooney amesema: "Nilipokuwa nikikua huko Croxteth, Duncan Ferguson alikuwa shujaa wangu. "
Rooney ameongeza: "Njia bora ya kumshukuru Duncs kwa yote
aliyonifanyia mimi ni kuja kucheza hii Mechi ya kumuenzi. Hata kama
asingeniita kuja kucheza ningekuja kumshukuru!"
Duncan Ferguson ni mmoja wa Malejendari wa Everton aliyoichezea kwa
vipindi vitatu tofauti kuanzia Mwaka 1994, alipokuwa kwa Mkopo kutoka
Rangers ya Scotland, 1994 hadi 1998 na 2000 hadi 2006.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni