tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

31 Agosti 2015

HIZI NDIO DHAHABU ZA MSIMU ULIOPITA ZILIZOGEUKA MAKAA YA MAWE MSIMU HUU…

chelsea
 
Nikiwa nimekaa kwenye kiti changu cha mbao maarufu kama ‘benchi’ nilishangaa sana kuona umati wa watu ukishangilia goli la kichwa cha kufunika cha Andrew Ayew, binafsi sikushangilia kwani bado nilikuwa nasikia harufu ya damu.
Japokuwa Montero hakuwepo ila bado niliamini lazima shetani achinjwe tena kifo kibaya hasa kutokana na uwepo wa Bafetimbi Gomis pale mbele. Kabla sijaisoma ‘sms’ iliyoingia kwenye simu yangu niliona pasi ya Ayew inamfikia Gomis katikati ya mabeki wawili wa Van Gaal, kwakweli hadi sasa sijui kiliendelea nini….
Anyway tuachane na huo unafiki wa kisoka maana ndio raha yenyewe ya mchezo huu unaopendwa sana hapa duniani pengine kuliko michezo yote. Soka ni mchezo wa ajabu sana kwani maajabu pia yana nafasi yake katika tasnia hii. Msimu uliopita kuna baadhi ya timu zilianza vyema sana ila msimu huu mambo yamebadilika sana hadi watu wanashika vichwa. Hapa chini nimekuweeka timu ambazo zilianza vyema ila msimu huu mabo
magumu kama chaguzi za wanachama wa TFF huko mikoani, karibu sana…
BORUSSIA MONCHENGLADBACH
Msimu uliopita Borussia Monchengladbach walishika nafasi ya tatu huku wakitoa changamoto kibao licha ya kutolewa mapema kwenye michuano ya Europe League. Usajili waliofanya inawezekana uliwapa kitu cha ziada
jamaa hawa ambao wapo kundi moja na Man City. Katika mechi tatu za mwanzo msimu 2014/15, Monchengladbach hawakufungwa mechi hata moja licha ya kuanza kwa sare mbili dhidi ya VfB Stuttgart na SC Feiburg kabla ya kuirarua Schalke 04 mabao 4-1 na kukamilisha pointi tano kwenye mechi tatu.
Msimu huu timu hii imeanza vibaya sana kwani katika mechi tatu hadi sasa haijapata ushindi wala sare yeyote. Monchengladbach ndiyo timu inayoshikilia mkia katika mechi tatu za Bundesliga hadi sasa.
Walianza kwa kipigo cha 4-0 kutoka kwa Dortmund, kichapo cha 2-1 nyumbani kutoka kwa Mainz 05 kabla ya kulala 2-1 juzi kutoka kwa Weder Bremen. Tayari imeruhusu magoli nane hadi sasa bila pointi yoyote. Japokuwa bado ni mapema ila wanapaswa kujipanga upya mapema.
JUVENTUS
Msimu uliopita timu ya Juventus ilianza kwa kasi kama ilivyofanya pia misimu ya nyuma kabla ya msimu huo. Utakumbuka Juventus walimaliza ligi kwa kukusanya pointi 87 huku pia wakifanya vizuri kwenye ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Juve walishinda mechi zao tatu za mwanzo kwani walianza kwa ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Chievo kabla ya kuirarua Udinesse 2-0 na kuwamaliza kabisa Milan 1-0 pale Sansiro. Matokeo haya yalidhihirisha beki bora ya Juventus kwa kutoruhusu goli ndani ya mechi hizi.
Msimu huu, Juventus wameanza vibaya sana tena zaidi ya sana. Kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa AS Roma kilikuwa ni mwendelezo wa kile cha 1-0 kutoka kwa Udinese nyumbani. Hali hii inawafanya mabingwa hawa wa Italia kukamilisha mechi hizi bila pointi yoyote kitu ambacho sio kawaida.
Mechi ijayo wanacheza na Chievo Verona nyumbani, Massimiliano Allegri anasubiriwa kwa hamu kuona kama ataweza kuchukua pointi tatu kwa mara ya kwanza ndani ya msimu huu.
OLYMPIC MARSEILLE
Olympic Marseille ni timu nyingine ambayo vyombo vingi vya habari haviangalii mwenendo wake wa msimu uliopita na msimu huu inawezekana ni kwa sababu ya kutekwa na Uingereza na Uhispania. Msimu uliopita timu hii ilishika nafasi ya nne kwa kuwa na pointi 69.
Katika mechi zake nne za mwanzo, Marseille ilikusanya pointi sba kati ya 12. Marseille ilitoa vipigo kwa Guingamp na Nice baada ya kutoa sare na Bastia kabla ya kipigo cha 2-0 kutoka kwa Montpellie. Pointi saba zilikuwa muhimu sana kwao.
Msimu huu watu walidhani kwamba timu hii itarejesha makali yake lakini imekuwa ndivyo sivyo japokuwa ni mapema sana kuwahukumu ndani ya mechi nne za French League 1. Ndani ya mechi hizi timu hii imekusanya pointi tatu pekee huku ikipoteza mechi tatu kwa kupigwa na Caen, Reims na Guingamp. Japokuwa walishinda magoli sita kwa Troyes mechi iliyopita kabla ya jana ila bado jana walipokea kipigo ugenini. Mwanzo huu bado sio mzuri kwa timu hii inayonolewa na Marcelo Bielsa.
CHELSEA FC
Timu hii ilianza kwa kasi sana msimu uliopita kwa kutoa dozi kwa kila aliyekutana nae muda wowote. Utakumbuka Chelsea ya mwaka jana ilikuwa inapewa nafasi ya kumaliza ligi bila kupoteza mechi kabla ya
kusimamishwa na Newcastle kwa mara ya kwanza. Blues walikusanya pointi 12 kwenye mechi nne za mwanzo dhidi ya Burnley, Leicester, Everton na Swansea huku ikiruhusu magoli sita na kufunga magoli 15 ya haja. Matokeo haya yalifanya wachambuzi waipe nafasi tena Chelsea msimu huu.
Msimu wa sasa mambo ni magumu kwa vijana hawa wa Mourinho kwani wamefanya madudu ya kutosha baada ya kuruhussu magoli tisa ndani ya mechi nne huku wakifunga magoli sita pekee. Hadi sasa Chelsea ina pointi nne kati ya 12 walizopaswa kukusanya. Chelsea imeshinda mechi moja pekee tena
kibahati kwani walikuwa wanaomba mpira uishe. Jose Mourinho anapaswa kuchanga karata zake vyema kwani ana mechi ngumu zinazomkabili na asipoangalia ataanza kunyooshewa vidole na Abromovich. 

Hakuna maoni: