tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

31 Agosti 2015

MARTIAL ATUA OLD TRAFFORD, CHICHA, JANUZAJ WAKIMBILIA GERMANY, BORINI AIHAMA ANFIELD!

WAKATI Straika Chipukizi wa France Anthony Martial akiwa hatua za mwisho kutua rasmi Manchester United, Wachezaji wa Klabu hiyo, Javier Hernandez ‘Chicharito’ na Adnan Januzaj, wako mbioni kuhamia Germany huku Straika wa Liverpool, Fabio Borini, akiuzwa kwa Sunderland.
MARTIAL ATUA OLD TRAFFORD
ANTHONYMARTIALStraika wa AS Monaco Anthony Martial yuko hatua za mwisho kukamilisha uhamisho wake kwenda Manchester United kwenye Dili ya Pauni Milioni 36 ambayo itamfanya awe Tineja wa Bei ghali mno.
Hivi sasa Kijana huyo wa Miaka 19 ambae ameitwa Kikosi cha Timu ya Taifa ya France anafanyiwa upimwaji afya yake huko Man United.
Wadau wengi wa Man United wamekuwa wakijiuliza Anthony Martial ni nani lakini ni Kijana Fowadi hatari ambae anafananishwa na Thierry Henry kiasi cha Kocha wa France Didier Deschamps kuamua kumwita Timu ya Taifa.
Martial alianza Soka lake kwenye Chuo cha Soka cha Lyon na kuichezea Timu ya Kwanza Mechi 3 kisha kuhamia AS Monaco Mwaka 2013 kwa Pauni Milioni 3.6.
Msimu uliopita, Martial ndio aling’ara sana na kuipigia AS Monaco Bao 11.
Moja ya Mechi zake alizowika ni ile ya waliyoibwaga Arsenal nje ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa kuichapa 3-1 huku Martial akimgeuza atakavyo Hector Bellerin.
Hata UEFA, kwenye Ripoti yao ya Ufundi ya Mwaka 2013, kufuatia Fainali za EURO 2013 kwa U-21, ilimtambua na kumtaja kuwemo katika Kikosi Bora cha Mashindano hayo.
ADNAN JANUZAJ AKOPESHWA BORUSSIA DORTMUND!
Winga wa Manchester United Adnan Januzaj yupo katika mazungumzo ya mwisho na Borussia Dortmund ili kukamilisha Uhamisho wa Mkopo wa Mwaka mmoja.
Chini ya Meneja Louis Van Gaal, Januzaj amekuwa si chaguo la Meneja huyo na sasa ameamua kwenda Bundesliga kwa Mkopo ilia apate namba.
JAVIER HERNÁNDEZ ‘CHICHARITO’ AUZWA LEVERKUSEN!
NaeJavier Hernandez ‘Chicharito’ sasa yupo mbioni kumaliza Miaka yake Mitano na Manchester United kwa kuhamia Klabu ya Germany Bayer Leverkusen kwa Dau linalokadiriwa kuwa Pauni Milioni 8.75.
Msimu uliopita Chicharito alikuwa huko Real Madrid kwa Mkopo na Msimu huu kurudi tena Old Trafford lakini amekuwa hana namba na kununuliwa kwa Anthony Martial kutoka AS Monaco ndiko kunamwondoa.
LIVERPOOL YAMUUZA FABIO BORINI
Nao Liverpool wameikubali Ofa ya Pauni Milioni 10 kumnunua Mchezaji wa Kimataifa wa Italy Fabio Borini.
Borini, mwenye Miaka 24, aliichezea Sunderland kwa Mkopo katika Msimu wa 2013/14 na kuifungia Bao 7 katika Mechi 32.
Borini amekuwa pia akisakwa na Inter Milan, Fiorentina na Watford lakini hakuna hata mmoja aliefikia Dau ambalo Liverpool walikuwa wakilitaka.
Borini ndie alikuwa Mchezaji wa kwanza kabisa kwa Meneja Brendan Rodgers kumsaini mara tu aliposhika wadhifa wake Klabuni Liverpool kwa kumnunua kutoka AS Roma Julai 2012 kwa Dau la Pauni Milioni 11.
Akiwa na Liverpool, Borini amefunga Bao 3 katika Mechi 38

Hakuna maoni: