tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

19 Septemba 2015

BENITEZ AMPA SOMO RONALDO

Benitez RonaldoKocha Rafael Benitez wa Real Madrid ya uhispania amesema Ronaldo ni mchezaji muhimu zaidi kikosini hapo lakini akamtaka kutumia kipaji chake kwa manufaa zaidi ya timu kuliko tuzo binafsi.
Benitez aliyasema hayo alipoulizwa kwamba ni mchezaji gani wa Madrid anamfananisha na Paul Gasol mchezaji wa kikapu aliyeifungia Spain points 40 dhidi ya Ufaransa katika nusu fanali na kuiingiza Spain fainali ya kikapu barani Ulaya.
Benitez alijibu kwamba, Ronaldo ndio Gasol wao, lakini akamtaka mchezaji huyo bora wa dunia kutumia kipaji chake kwa ajili ya timu. Akitolea mfano, anasema Gasol alicheza kitimu na ndio sababu ameisaidia Spain kuingia fainali.
Kulikua na kutokuelewana sana baina ya Ronaldo na kocha Rafael Benitez ambaye kwasasa anaonekana kupata ubora wa Ronaldo ambaye amefunga magoli 8 katika mechi mbili za mwisho za Real Madrid.
Kuhusiana na alichoandika Steven Gerrard katika kitabu chake kwamba Benitez alikua hampendi Gerrard, Benitez anasema kwa heshima aliyonayo kwa mashabiki wa Liverpool, na muda mzuri waliokua nao na Steven Gerrard, hawezi kumuongelea Gerrard kwa ubaya hata mara moja.
Akiulizwa kuhusu lini Gareth Bale atarudi dimbani baada ya kuumia, Benitez anasema haiwezi kuwa haraka kiasi hiki na inawezekana Bale akakaa nje ya uwanja kwa takribani wiki tatu.

Hakuna maoni: