WENGER ATAKA FA ICHUNGUZE KWA NINI DIEGO COSTA HAKUPEWA KADI NYEKUNDU!
Rai hiyo imetolewa na Meneja wa Arsene Wenger lakini imepingwa vikali na Meneja wa Chelsea Jose Mourinho aliemtaka Wenger aache kulalamika kila mara.
Katika Mechi hiyo, Sentahafu wa Arsenal Gabriel alitolewa kwa Kadi Nyekundu baada ya kumtia Teke Costa na baadae Kipindi cha Pili Arsenal walibaki Mtu 9 baada ya Kiungo wao Santi Cazorla kupewa Kadi za Njano 2 na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Wenger amesema: “Huyu Costa atafanya hivi hivi Wiki ijayo na Wiki inayofuata na Siku zote hukwepa Kadi!”
Wenger alieleza: “Siku zote Costa anafanya anachotaka na anabaki Uwanjani lakini wengine wote wakijibu uchokozi wake wanatolewa nje. Alimpiga Koscielny usoni na hakufanywa kitu. Costa ametumia udhaifu wa Refa Mike Dean.”
Lakini Jose Mourinho amejibu tuhuma hizo za Wenger kwa kudai Wenger Siku zote hulalamika tu: “Nimechezea na Wenger mara 15 na mara pekee hakulalamika ni tulipofungwa kwenye Ngao ya Jamii!”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni