BUNDESLIGA: JUMANNE BAYERN NA WOLFSBURG, JUMATANO HOFFENHEIM NA DORTMUND!
Jumanne, Bayern Munich wako kwao Allianz Arena kucheza na VfL Wolfsburg ambao wako Nafasi ya 3 baada ya kushinda Mechi 3 na Sare wakiwa na Pointi 11 zikiwa ni Pointi 4 nyuma ya Bayern ambao wako Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 15 sawa na Vinara Borussia Dortmund.
Msimu huu, Wolfsburg, ambao ndio waliobeba German Cup, walishaifunga Bayern Munich Mwezi Agosti baada ya kuwabwaga kwa Penati kwenye Mechi ya kufungua pazia Msimu mpya ya kugombea Super Cup.
Nao Borussia Dortmund Jumatano wapo Ugenini kucheza na Hoffenheim wakisaka ushindi wao wa 6 mfululizo kwenye Bundesliga.
BUNDESLIGA
RATIBA
**Saa za Bongo
Jumanne Septemba 22
2100 Bayern Munich v VfL Wolfsburg
2100 Hertha Berlin v Cologne
2100 Ingolstadt v Hamburg
2100 Darmstadt 98 v Werder Bremen
Jumatano Septemba 23
2100 Schalke 04 v Eintracht Frankfurt
2100 Bayer Leverkusen v Mainz
2100 Borussia Moenchengladbach v Augsburg
2100 Hanover 96 v VfB Stuttgart
2100 Hoffenheim v Borussia Dortmund
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni