CHICHARITO AMPOTEZEA VAN GAAL, AAGA MASHABIKI, AMKUMBUKA FERGUSON
Javier
Hernandez ‘Chicharito’ kushoto akiwa katinga uzi wa klabu yake mpya
(kulia) ni mgurugenzi wa michezo wa Bayer Leverkusen Rudi Voller
Mshambuliaji raia wa Mexico,
Javier Hernandez ‘Chicharito’ ametoa salamu zake za mwisho za kuaga
Manchester United huku akiwashukuru kocha Sir Alex Ferguson, mkuu wa
maskauti Jim Lawlor pamoja na mashabiki, huku akiwapotezea kocha wa sasa
wa Manchester United, Louis Van Gaal pamoja na aliyekua mrithi wa
Ferguson, David Moyes.
Kupitia katika kurasa zake za
mitandao ya kijamii Hernandez ambae alisajiliwa kujiunga na Manchester
United mwaka 2010 akitokea Guadajala ya nyumbani kwao Mexico,
amemshukuru kwa nafasi ya pekee mkuu wa maskauti wa Manchester United
ndugu Jim Lawlor kwa kumsaidia kujulikana na dunia.
Aidha amempa sifa zake kocha
legendari wa Manchester United, mstaafu Alex Ferguson kwa kumkuza kama
mwanae huku akisema pia hatowasahau mashabiki wa Manchester United.
Hernandez hivi sasa amejiunga na
klabu ya soka ya Bayern Leverkusen na kusisitiza amefurahi kuwa sehemu
ambapo anaonekana ni mtu muhimu. Chicharito ambaye tangu kustaafu kwa
kocha Alex Ferguson, alikua katika wakati mgumu kwenye klabu ya
Manchester United chini ya walimu David Moyes na Louis Van Gaal.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni