tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

3 Septemba 2015

MADINI ADIMU USIYOYAJUA KUTOKA KWA BEKI MPYA WA CHELSEA PAPY DJILOBODJI

Papy-Djilobodji
Na Salym Juma 
Mimi sio miongoni mwa mashabiki wa Chelsea na sina timu kabisa Uingereza, kila siku nawaambia timu yangu ni ‘BvB’ naamini wale wazee wa Bundesliga mnaifahamu timu hii. Japokuwa sina timu ila kuna vitu vinanifurahisha pale na vingine vinanihuzunisha sana pale EPL. Bafetimbi Gomiz na Wayne Rooney wananifurahisha sana kutokana na viwango vyao! Najua kuna watu nawagusa hapa ila ‘CYBER CRIME’
inanilinda. Ivanovic na Pedro wananipa raha sana kutokana na viwango yao matata…! Najua kuna watu wamekunja uso hapa, Anyway mtajua wenyewe ila ‘Unafiki’ siachi ng’oo…….
“Ni mara chache sana nimekutana na beki anayetumia miguu yote na anacheza vizuri kwa kutumia miguu hii” Yaya Toure.
Kama wewe ni mpenzi mzuri wa mipira ya Kia-afrika utakuwa unafahamu kauli hii ya mchezaji huyu aliitoa wapi na lini. Kutokana na mapungufu yaliyopo kwenye idara ya ulinzi ya Chelsea, hivi karibuni Jose
Mourinho alinasa saini ya mchezaji mkubwa mwenye jina dogo, anayecheza ligi ndogo na timu isiyojulikana kabisa kwa watu walioujua mpira karibuni. Naamini wengi mnafahamu mchezaji wa Kisenegali ndiye anayezungumziwa hapa na sio mwingine bali ni Papis Mison Djilobodji, kijana mwenye miaka 26 aliyetua kuimarisha idara ya ulinzi ya Chelsea.
Kutokana na usaili huu kuzungumzwa sana mitaa mbalimbali ya nchi hii ambayo anatokea msanii mkubwa Afrika anayeitwa Diamond Platnum, leo hii nimekuletea vitu adimu ambavyo pengine huvijui kutoka kwa mchezaji huyu aliyecheza mechi 13 kwenye timu yake ya taifa. Karibu sana…
BEKI MKAKAMAVU NA MGUMU PALE NYUMA
Unapozungumzia mabeki hodari kwenye ligi kuu ya Ufaransa huwezi kumuacha mlinzi huyu japokuwa hakutajwa sana kutokana na majina ya akina David Luis na Thiago Silva kuwa maarufu kwenye vinywa vya wanasoka wengi hasa wale walioanza kufuatilia mpira miaka ya hivi karibuni. Papy Djilobodji (26) ni beki mzuri sana anayehitajika na kocha makini kama Jose Mourinho ila kinachomgharimu ni umri pekee kwani Mou alihitaji beki mwenye chini ya miaka 23 ili aweze kutengeneza ‘Partnership’ na akina Kourt Zouma, Baba Rahman na Cesar Azipilicueta.
Papy kama beki makini ana wastani wa kufanya ‘Clearance’ 8.3 kwa mechi moja, pia amefanya ‘Interception’ 3.3 kwa mechi moja na huu ni wastani mzuri sana. Pia kafanya jumla ya ‘Interception’ 101 na kumfanya kuwa juu katika kipengele hiki kuliko beki yoyote wa Chelsea. Papy pia akiwa kama Mlinzi pale nyuma, licha ya timu yake kumaliza nafasi ya 14, waliruhusu magoli 40 ndani ya mechi 38 za ligi. Sasa itakuaje kama atacheza sambamba na mabeki wa kiwango cha dunia pale nyuma? Kwa takwimu hizi ni wazi tusubiri makubwa kutoka kwake.
ANATUMIA MIGUU YOTE, MREFU NA MWEPESI SANA
Msenegali huyu ana faida tatu tajwa hapo juu. Nguvu pia ni faida nyingine ambayo kijana huyu anayo na hatimaye kuwa tofauti na wachezaji wengine. Urefu wake ni futi 6 na inchi 4, kutokana na hili jamaa ana wastani mzuri sana wa kupiga mipira ya juu hasa ile ya vichwa pindi inapokuwa langoni mwake na kwenye goli la wapinzani pia. Papy ana wastani wa kuokoa mipira ya vichwa kwa 3.1 katika mechi moja. Pia jamaa anatumia miguu yote na hivo anaweza kucheza nafasi zote kama Mdogo wangu Cesar Azipilicueta. Wepesi wake utamfanya afanye makubwa sana pale Darajani.
NI MCHEZAJI HODARI ANAYEWEZA KUCHEZA NAFASI TOFAUTI
Kama nilivyotanguia kukuambia hapo kabla kuwa huyu jamaa anatumia miguu yote miwili, hivyo anaweza kucheza nafasi zote kati ya zile 4 za pale nyuma. Papy pia anaweza kucheza kama ‘Defensive-midfielder’ na wakati mwingine pia anaweza kucheza kama ‘Holding-midfielder’ Kama wewe ni mfuatiliaji wa mbinu za Jose Mourinho utakubaliana na mimi kuwa Mou anapenda wachezaji wanaoweza kubadili nafasi Zaidi ya moja uwanjani kama akina Ramos, David Luiz, Pepe na wachezaji wenye kaliba ya akina Nemanja Matic.
NI MFUNGAJI MZURI PALE ANAPOPATA NAFASI
Kutokana na urefu, wepesi na ujanja wa Mchezaji huyu ni wazi kuwa analijua goli hasa kutokana na takwimu zake za kufunga magoli tisa ndani ya mechi  171 kwenye Klabu yake ya Nantes. Magoli haya ni mengi mno
kwani kuna mabeki kibao pale Chelsea na timu zingine wamecheza mechi kibao bila kuwa na magoli kama haya. Papy ni mzuri sana kwenye mipira ya kona na ile ‘Free kick’ kwani anafahamu goli lilipo na ni mzuri pia ‘Kuji-position’ wakati mipira hii inapigwa. Inawezekana akafanya makubwa sana endapo ataaminiwa na Mou kwani ni mchezaji mzuri mno.
KACHELEWA SANA KUPANDA NDEGE
Ndege ninayoizungumzia hapa ni ile ya kuvuka bahari kwenda barani Ulaya. Papy kwa mara ya kwanza alikwenda Ulaya akiwa na miaka 19 hasa baada ya kuonekana ni mchezaji mzuri ila kama ilivyo kawaida, changaomoto katika maisha in kitu cha lazima kwani Papy licha ya kiwango chake alifeli majaribio kwenye Vilabu vya Lazio na Lile na hatimaye kuangukia kwenye timu ndogo ya Senart Moissy iliyokuwa daraja la nne pale Ufaransa. Hali hii haikumkatisha tamaa kwani alichez kwa bidii na kufikia hatua ya kusajili ligi kuu ya Ufaransa na sasa ni anakwenda Chelsea.

Hakuna maoni: