COUTINHO WA LIVERPOOL ANUKIA BARCELONA
Hali hiyo imekuja baada ya Neymar wa Barcelona kuulizwa ni mchezaji gani wa taifa lake angependa ajiunge naye mjini Catalunya, Neymar bila kusita alimtaja Coutinho kuwa itakua ni usajili mzuri kwa klabu na pia kwa mchezaji mwenyewe.
Mchezaji mwingine aliyetoka Liverpool, Luis Suarez naye ni moja ya wachezaji wanaomkubali sana Coutinho na wakati akiondoka Liverpool msimu wa 2014/15 alimuomba nahodha Steven Gerard kumpa uangalizi Coutinho.
Taarifa hizi sio nzuri kwa mashabiki wa Liverpool ambao wamekua wakishuhudia kuondoka mfululizo kwa mastaa wake akianzia Luis Suarez na msimu huu Raheem Sterling.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni