FERGUSON AWATAJA WANNE BORA KUWAHI KUWAFUNDISHA
Alex Ferguson amemtaja Cristiano Ronaldo kuwa ndiye mchezaji bora zaidi kuwahi kumfundisha huku akiwaongeza Erick Cantona, Ryan Giggs na Paul Scholes kama wachezaji wake bora wa kiwango cha dunia.
Lakini Fergie anasema aliowataja, wamethibitisha ubora wao huku akimwagia sifa Ryan Giggs kwamba atakuja kuwa ni kocha mkubwa na mafanikio mengi siku moja.
Akiongea kuhusu kitu anachokijutia katika maisha yake ya ukocha, Fergie anasema ni kutokushinda mataji mengi ya Ulaya ingawa alishinda makombe mbalimbali ya nyumbani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni