tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

1 Septemba 2015

DILI DE GEA KWENDA REAL YAKWAMA SEKUNDE ZA MWISHO!

DEGEA-NAVASUHAMISHO wa Pauni Milioni 29 wa Kipa David De Gea kutoka Manchester United kwenda Real Madrid umekwama Dakika za mwisho baada ya Mikataba yake kutokamilika kwa wakati.
Tatizo kubwa ni kuwa Dirisha la Uhamisho huko Spain lilifungwa Jana Saa 7 za Usiku kwa Saa za Tanzania wakati lile la Uingereza Leo ndio mwisho wake, hapo Saa 2 Usiku kwa Saa zetu.
Uhamisho huu wa De Gea ulihusu Kipa huyo kwenda Real na Klabu hiyo ya Spain kuilipa Man United Pauni Milioni 29 pamoja na kumtoa Kipa wao kutoka Costa Rica, Keylor Navas, kwa Man United.
Hivi sasa kila Klabu imebaki kimya lakini ripoti kutoka huko Spain zinadai kuwa Man United ndio waliochelewesha kukamilisha Uhamisho huo kwa kutuma Mkataba uliosainiwa Dakika 1 baada ya Dirisha la Uhamisho kufungwa hapo Saa 7 na Dakika 1 Usiku.
Hata hivyo, habari toka ndani ya Man United zinadai kuwa wanayo Risiti inayoonyesha kuwa Makabrasha yote yalitumwa kwa wakati.
Ikiwa ukweli ni kuchelewa kwa Makabrasha kufika huko Spain kwa wakati basi kilichobaki ni Real kukata Rufaa kwa FIFA ambao ndio wanahusika kwa Uhamisho wa Kimataifa.
Bila hivyo David De Gea atabakia Man United kwa Msimu zaidi hadi Mkataba wake umalizike mwishoni mwa Msimu huu wa 2015/16.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
HABARI ZA AWALI:
NI MALI KWA MALI - DE GEA YU REAL, NAVAS PAMOJA NA £29.3M NDANI MAN UNITED!
WAKATI Dirisha la Uhamisho likifungwa Usiku huu huko Spain, Real Madrid wamefanikiwa kumnasa Kipa wa Manchester United David De Gea.
Lakini, Real, kwa mujibu wa ripoti za ndani, wanatakiwa wamtoe Kipa wao kutoka Costa Rica, Keylor Navas, kwa Man United na pia kulipa Dau la Pauni Milioni 29.3 kwa Man United nah ii inaifanya Man United kufaidika hasa kwa kumuuza Mchezaji ambae amebakisha Mwaka mmoja tu katika Mkataba wake.
Dili hii kwa Man United hii Leo ni ya pili baada ya pia kumchukua Straika Chipukizi wa France, Anthony Martial, kutoka AS Monaco na pengine huenda Jumanne, ambayo ndio Dirisha la Uhamisho linafungwa huko England, wakafanya biashara nyingine kama minong’ono inavyokwenda.
Sakata la De Gea kuhamia Real limedumu kwa kipindi kirefu baada ya Kipa huyo kukataa kusaini Mkataba mpya ulioboreshwa na Meneja wa Man United Louis van Gaal kuamua kutomwita Kikosini katika Mechi zao zote za Msimu huu mpya ulioanza Agosti 8.
Kwenye Mechi zote za Man United Msimu huu, Kipa wa Kimataifa wa Argentina, Sergio Romero, ndio amekuwa akidaka lakini ujio wa Keylor Navas, ambae aling’ara mno wakati wa Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwaka Jana akidakia Costa Rica, kutaleta ushindani mkubwa.
Real walimnunua Navas toka Levante kwa Dau la Pauni Milioni 7 mara tu baada ya Fainali za Kombe la Dunia kumalizika.

Hakuna maoni: