HIZI NI SABABU KUMI ZA KUILAUMU MANCHESTER UNITED BAADA YA DE GEA KUSHINDWA KWENDA REAL MADRID
Ndoto ya De Gea kwenda Real Madrid kwa gharama ya £29m imeota manyoya. Mazungumzo yalifunguliwa kati ya Real Madrid na Manchester United jana lakini mambo hayakwenda vizuri. Kwenye hili dili ilibidi golikipa Keylor Navas ajiunge na Manchester ikiwa ni sehemu ya kubadilishana. De Gea ilibidi asajiliwe kwa mkataba wa miaka 6 na Real Madrid, lakini Real wanailaumu Manchester kwa kuchelewesha mipango yao.
Hizi ni sababu 10 ambazo Real Madrid wamezitaja kuwalaumu Manchester kuhusu usajili wa De Gea.
1)Manchester United hawakufungua mazungumzo hadi siku za mwisho asubui ndio waliungua mazungumzo
2)Real Madrid licha ya kujua kwamba kuna ugumu kwenye kukamilisha hili dili walianzisha mazungumzo kati yao.
3)Siku yaku ya Jumatatu ambapo Manchester walifungua ishu ya makubaliano ilibidi mambo yote yakamilike wakati kati ya Keylor Navas na wawakilishi wa wachezaji lakini haikua hivyo.
4)Madrid na United walikubaliana kwa haraka kuhusu uhamisho na likabaki kwa club kutuma karatasi tu FIFA. Real wakatuma haraka karatasi lakini Manchester ndio walichelewesha
5)Manchester united walijibu makubaliano yao kwa makaratasi kwenda Real Madrid ikiwa na mabadiriko machache na Real Madrid ikakubaliana nayo.
6)Baada ya Real kupata sign ya David De Gea na Keylor Navas wakarudisha form Manchester haraka kwa lengo la kutaka zipate sign ya upande wa pili.
7)Manchester United walikubaliana na mwakilishi Keylor Navas kwa muda wa saa sita karoso usiku kwa masaa ya Hispania.
8)Manchester united wakaweka pamoja document zote kuhusu operation ya David De Gea kwa muda wa saa 6 usiku na kuzituma Real Madrid ili kwa mabadilishano ya document za kimkataba na huo muda ulikua 00:02 ambapo lwa Real Madrid muda wa transfer ulikua umeisha.
9)Saa 6 usiku na dakika 26 Real Madrid wakatuma document La Liga wakijua kwamba muda wa usajili kwao umeisha lakini kwa England bado unaendelea hadi leo.
10)Hadi mwisho wa mchakato Real Madrid walionekana kuwa wamefanya kila kitu lakini uchelewashwaji umefanyika na Manchester united.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni