tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

21 Septemba 2015

‘DOGO DENJA’-ANTHONY MARTIAL-BAO 3 MECHI 3, WATAISOMA NAMBA!

MANUNITED-MARTIAL-SHUJAAKWENYE Mechi yake ya kwanza tu ya Ligi Kuu England ambayo alianza tangu mwanzo, Anthony Martial amefunga Bao 2 wakati Manchester United inaicharaza Southampaton Bao 3-2 katika Mechi ya Jumapili ya Ligi Kuu England huko Saint Mary.
Mechi yake ya kwanza kabisa ya Ligi kwa Martial, Kijana wa Kifaransa wa Miaka 19 tu, ilikuwa huko Old Trafford hapo Septemba 12 ambapo aliingizwa toka Benchi na kupachika Bao murua wakati Man United inaitandika Liverpool 3-1.
Hapo Jana, huku Man United wakiwa Bao 1-0 nyuma walipocheza na Southampton, Martial, akicheza Sentafowadi, huku Kepteni Wayne Rooney akiwa nyuma yake, ndie aliesawazisha Bao na kisha kupiga Bao la pili na Man United kwenda Bao 2-1 mbele.
Bao la 3 la Man United lilifungwa na Juan Mata wakati Bao zote za Southampton zikifungwa na Graziano Pelle.
Akimwongelea Martial, Mchezaji wa zamani wa Southampton, Morgan Schneiderlin, ambae Jana alirejea Saint Mary kuikabili Timu yake ya zamani kwa mara ya kwanza, alisema: “Kama mlivyomwona, ni mtulivu, hana mchecheto. Ana kipaji kikubwa. Amekuja Ligi Kuu England na anafunga. Ni Mchezaji mwenye akili mno, alietulia. Atakuwa Mchezaji Bora mno kwa Man United!”
Nae Meneja wa Man United, Louis van Gaal, ameeleza: “Ni kweli ameanza vizuri lakini tatizo ana Miaka 19 tu na usitegemee kila Siku atacheza vyema lakini amecheza Mechi 3 mfululizo kwa kiwango cha juu na kufunga Mabao, na hilo ni muhimu!”
Jumatano Man United ipo Old Trafford kucheza Mechi ya Raundi ya 3 ya Capital One Cup dhidi ya Ipswich Town na Jumamosi ijayo wapo tena Old Trafford kuivaa Sunderland kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Huenda Mashabiki, ambao sasa wameanza kuwakebehi wapinzani walipochekwa kwa Bei mbaya aliyonunuliwa Martial, wakaendelea kujigamba-WATAISOMA NAMBA! 

DIEGO COSTA-FA YANGOJA RIPOTI YA REFA DEAN ILI KUMSULUBU!

ARSENAL-GABRIEL-RCFA, Chama cha Soka England, kinasubiri kupokea Ripoti ya Refa Mike Dean hapo Jumatatu ili kuamua kama watamchukulia hatua Straika wa Chelsea Diego Costa ambae alikuwa chanzo cha vurumai zilizosababisha Beki wa Arsenal Gabriel Paulista kutolewa kwa Kadi Nyekundu.
Costa alikuwa kiini cha mzozo baada ya kumpiga usoni na kisha kumwangusha chini Beki wa Arsenal Laurent Koscielny wakati wa Mechi iliyochezwa Jumamosi huko Stamford Bridge na Chelsea kuifunga Arsenal 2-0.
Lakini Refa Mike Dean aliamua kuwapa Kadi za Njano wote wawili, Costa na Koscielny, badala ya Kadi Nyekundu kwa Costa kama wengi walivyotarajia.
Mara baada ya tukio hilo ndipo Costa na Paulista wakaanza kuzozana na ndipo Paulista akamfyatua Teke Costa na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Ikiwa Refa Mike Dean atabainisha katika Ripoti yake kuwa aliliona tukio lote la Costa na Koscielny na kuamua ni la Kadi ya Njano basi huenda Costa akanusurika Rungu la FA.
Lakini ikiwa Refa Dean atasema hakuona tukio lote basi ni wazi Adhabu kali itamkabili.
HABARI ZA AWALI:
WENGER ATAKA FA IMCHUNGUZE COSTA!
Chama cha Soka England, kimetakiwa kichunguze kwa nini Straika wa Chelsea Diego Costa ameepuka kupewa Kadi Nyekundu katika Mechi yao ya Ligi Kuu England iliyochezwa Leo Stamford Bridge na Chelsea kuifunga Mtu 9 Arsenal Bao 2-0.
Rai hiyo imetolewa na Meneja wa Arsene Wenger lakini imepingwa vikali na Meneja wa Chelsea Jose Mourinho aliemtaka Wenger aache kulalamika kila mara.
Katika Mechi hiyo, Sentahafu wa Arsenal Gabriel alitolewa kwa Kadi Nyekundu baada ya kumtia Teke Costa na baadae Kipindi cha Pili Arsenal walibaki Mtu 9 baada ya Kiungo wao Santi Cazorla kupewa Kadi za Njano 2 na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Wenger amesema: “Huyu Costa atafanya hivi hivi Wiki ijayo na Wiki inayofuata na Siku zote hukwepa Kadi!”
Wenger alieleza: “Siku zote Costa anafanya anachotaka na anabaki Uwanjani lakini wengine wote wakijibu uchokozi wake wanatolewa nje. Alimpiga Koscielny usoni na hakufanywa kitu. Costa ametumia udhaifu wa Refa Mike Dean.”
Lakini Jose Mourinho amejibu tuhuma hizo za Wenger kwa kudai Wenger Siku zote hulalamika tu: “Nimechezea na Wenger mara 15 na mara pekee hakulalamika ni tulipofungwa kwenye Ngao ya Jamii!”

Hakuna maoni: