tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

21 Septemba 2015

LA LIGA: MESSI AKOSA PENATI, APIGA 2, BARCA KILELENI!

MESSI-SHANGILIA-BARCAMABINGWA Watetezi wa La Liga, FC Barcelona, wameendelea kujikita kileleni mwa Ligi hiyo ya Spain baada ya Jana Usiku wakiwa kwao Nou Camp kuichapa Levante Bao 4-1.
Licha ya kukosa Penati katika Dakika ya 75, Lionel Messi alifunga Bao 2, moja likiwa pia Penati ya Dakika ya 61 na jingine kwenye Dakika ya 90.
Bao nyingine za Barca zilifungwa na Marc Bartra Dakika ya 50 na NeymarLALIGA-STAND-SEP21Dakika ya 56.
Bao pekee la Levante lilifungwa na Victor Casadesus katika Dakika ya 66.
Ushindi huu umewafikisha Barcelona Pointi 12 baada ya kushinda Mechi zao zote 4 na kuongoza La Liga wakifuatiwa na Real Madrid wenye Pointi 10 wakiwa wamefungana kwa Pointi na Villareal na Celta Vigo.
La Liga itaendelea tena kati ya Wiki kwa Mechi za Jumanne, Jumatano na Alhamisi.
VIKOSI:
Barcelona (Mfumo 4-3-3): Ter Stegen; Alves, Bartra, Mascherano, Adriano; Busquets, Rakitic, Munir; Messi, Sandro, Neymar
Akiba: Masip, Alba, Mathieu, Sergi Roberto, Iniesta, Gerard Gumbau, Suarez.
Levante (Mfumo 5-3-2): Ruben; Ivan, Trujillo, Feddal, Juanfran, Tono; Camarasa, Lerma, Verza; Ghilas, Roger
Akiba: Marino, Karabelas, Jose Mari, Deyverson, Ruben Garcia, Morales, Victor Casadesus.
REFA: David Fernandez Borbalan
LA LIGA
RATIBA/MATOKEO:
**Saa za Bongo
Ijumaa Septemba 18
Getafe CF 1 Malaga CF 0
Jumamosi Septemba 19
Real Madrid CF 1 Granada CF 0
Valencia C.F 0 Real Betis 0
SD Eibar 0 Atletico de Madrid 2
Real Sociedad 2 RCD Espanyol 3
Jumapili Septemba 20
Sevilla FC 1 Celta de Vigo 2
Deportivo La Coruna 2 Sporting Gijon 3
Villarreal CF 3 Athletic de Bilbao 1
FC Barcelona 4 Levante 1
Las Palmas 0 Rayo Vallecano 1
Jumanne Septemba 22
2100 Atletico de Madrid v Getafe CF
2100  RCD Espanyol v  Valencia C.F      
2300  Granada CF v Real Sociedad       
Jumatano Septemba 23         
2100  Celta de Vigo v FC Barcelona       
2100  Rayo Vallecano v Sporting Gijon 
2100  Levante v SD Eibar 
2200  Athletic de Bilbao v Real Madrid CF       
2300  Malaga CF v Villarreal CF  
2300  Las Palmas v Sevilla FC     
Alhamisi Septemba 24         
2305  Real Betis v Deportivo La Coruna
Ijumaa Septemba 25
2130  Valencia C.F v Granada CF

Hakuna maoni: