KUELEKEA UEFA…AGUERO NJE YA KIKOSI CHA MAN CITY
Vinara wa EPL Manchester City
ya, leo wanatarajia kushuka dimbani kucheza mechi yake ya kwanza ya
hatua ya makundi ya klabu Bingwa barani Ulaya, dhidi ya ‘Kibibi kizee
cha Turin’, Juventus ya Italia, huo ukiwa ni mchezo wa kwanza wa kundi D
kwa klabu zote mbili.
Sergio Aguero ‘Kun’
Manchester City, tayari
wamethibitisha kumkosa mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina
anayekipiga klabuni hapo, Sergio Aguero ‘Kun’ baada ya kusumbuliwa na
jeraha la goti.
Aguero ataukosa mchezo huo,
baada ya kupata jeraha la goti katika mechi dhidi ya Crystal Palace,
mechi iliyomalizika kwa Man City kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
David Silva
Mshambuliaji huyo alipata
jeraha la goti baada ya kufanyiwa faulo mbaya na Scott Dann, hivyo
hatakuwepo katika mechi hiyo, pamoja na hali hiyo, kocha wa klabu hiyo
Manuel Pellegrini, amethibitisha kurejea kwa David Silva na Raheem
Sterling licha ya kukosa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Crystal Palace.
Raheem Sterling
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni