LIVERPOOL MRAMA: BRENDAN RODGERS-‘MCHECHETO WA MATOKEO MABOVU UNATUHARIBIA!’
- Created: Monday, 21 September 2015 05:36
Jumapili Ings aliingizwa kumbadili Christian Benteke wakati wa Haftaimu na Dakika 3 tu baadae akaipa Liverpool Bao walipocheza na Bournemouth katika Mechi ya Ligi Kuu England lakini Wageni hao wakapata Sare ya 1-1 kwa Bao la Russell Martin.
Matokeo hayo yamewafanya Liverpool kutoshinda katika Mechi zao 5 zilizopita na kuwaacha wakiwa na Pointi 8 tu kwa Mechi 6 za Ligi Kuu England.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
LIVERPOOL-Matokeo Mechi zao Msimu huuLigi Kuu England:
Agosti 2015
Ligi Kuu England: Liverpool 0-3 West Ham [29 Aug]
Ligi Kuu England: Arsenal 0-0 Liverpool [24 Aug]
Ligi Kuu England: Liverpool 1-0 Bournemouth [17 Aug]
Ligi Kuu England: Stoke 0-1 Liverpool [9 Aug]
Septemba 2015
Ligi Kuu England: Liverpool 1-1 Norwich [20 Sep]
Europa Ligi - Kundi B: Bordeaux 1-1 Liverpool [17 Sep]
Ligi Kuu England: Man United 3-1 Liverpool [12 Sep]
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Katika Mechi hiyo na Bournemouth, Brendan Rodgers alimtumia kwa mara ya kwanza baada ya Miezi Mitano Straika wake aliekuwa Majeruhi, Daniel Sturridge, lakini hilo halikuwapa ushindi.
Rodgers ameeleza: “Kwa sababu ya matokeo yetu ya hivi karibuni, Wachezaji wana mchecheto. Lakini Kipindi cha Pili tulijifungua na kucheza vizuri!”
Mechi inayofuata kwa Liverpool ya Ligi ni hapo hapo kwao Anfield hapo Jumamosi dhidi ya Aston Villa lakini Jumatano wapo pia Anfield kucheza Mechi ya Raundi ya 3 ya Capital One Cup dhidi ya Timu ya Daraja la chini Carlisle.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBALigi Kuu England:
**Saa za Bongo
Jumamosi Septemba 26
1445 Tottenham v Man City
1700 Leicester v Arsenal
1700 Liverpool v Aston Villa
1700 Man United v Sunderland
1700 Southampton v Swansea
1700 Stoke v Bournemouth
1700 West Ham v Norwich
1930 Newcastle v Chelsea
Jumapili Septemba 27
1800 Watford v Crystal Palace
Jumatatu Septemba 28
2200 West Brom v Everton
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni