MJUE ANTHONY MARTIAL ALIYESAJILI NA MANCHESTER UNITED
Anthony Martial ana miaka 19 amecheza soka kwenye Academy ya Lyon na amecheza mara tatu kwenye kikosi cha kwanza cha Lyon kabla hajaamia Monaco mwaka2013 kwa dau la £3.6m.
Kwenye msimu wake wa kwanza chini ya kocha Leonardo Jardim ameweza kufunga magoli 11 kwenye mashindano yote. Kwa wanaomkubwa alikua kwenye kikosi kilichoitoa Arsenal kwenye UEFA baada ya mechi iliyoisha 3-1 kwenye uwanja wa Emirates.
Martial aliwai kucheza na Falcao na pia alisema kwenye interview na BeIN sport kwamba anawaangalia sana Falcao na Manu Riviere ili kukua vizuri kwenye soka kwa sababu anawaona kila siku mazoezini.
Uhamisho wake kutoka Monaco kuja kwenye EPL unafananishwa na jinsi Thiery Henry mfaransa mwenzake alivyokuja kung’ara kwenye EPL. Sasa je na yeye atakua na njia kama Henry au vipi?
CEO wa Monaco aliwai kusema kwamba mchezaji huyu ana uwezo wa pekee wa ki-tecknical uwanjani, smart movement zinazoleta mdhara kwa timu pinzani”.Ligi ya uingereza ni tofauti sana na ligi yoyote duniani, haitabiriki kama ataweza kufanya vizuri au itakuaje?.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni