DIMARIA ATAJA KILICHOMUONDOA MANCHESTER UNITED
Baada ya kucheza kwa msimu mmoja
tu katika klabu ya Manchester United, winga Angel Di Maria amefunguka na
kumtaja kocha Louis Van Gaal kuwa ndiye sababu ya yeye kuondoka.
Akizungumza kupitia ESPN winga
huyo anayekipiga PSG hivi sasa anasema, “Van Gaal ana filosofia yake, na
ndio ilikua kikwazo kwangu. Nilifurahia maisha Old Trafford lakini
mambo yalibadilika baada tu ya kuumia ankle yangu na kocha kunibadilisha
nafasi ya kucheza uwanjani”.
Di maria anasema alishindwa
kuitumikia falsafa ya Louis Van Gaal na alipompigia simu Blanc (kocha wa
PsG) alimuhakikishia kumchezesha alivyokuwa akicheza Real Madrid.
Angel Di Maria aliweka rekodi ya
uhamisho kwa vilabu soka nchini England baada ya kusajiliwa kwa ada ya
uhamisho wa pauni milioni 60 akitokea Real Madrid
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni