UHAMISHO ENGLAND-MWISHO LEO: WEST HAM WANASA WATATU KWA MPIGO, MAN UNITED YAMPATA KINDA!
Leo Saa 2 Usiku kwa Saa za Bongo, Dirisha la Uhamisho huko England litafungwa na zifuatazo ni habari za nini kimejiri hadi sasa.UKURASA HUU UTAKUWA UKITOLEWA HABARI MPYA KADRI ZINAVYOKUSANYWA:
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
LIGI KUU ENGLAND-Biashara ya Leo Septemba 1
-Uhamisho wa Siku ya Mwisho
- Glenn Murray [Crystal Palace - Bournemouth] £4m
- Nikica Jelavic [Hull - West Ham] £3m
- Papy Djilobodji [Nantes - Chelsea] £4m
- Victor Moses [Chelsea - West Ham] Loan
- Ramiro Funes Mori [River Plate - Everton] £9.5m
- Alex Song [Barcelona - West Ham] Loan
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Virgil Van Dijk: Southampton kulipa Pauni Milioni 11.5 kwa Beki wa Celtic Southampton wamekubali kulipa
Beki huyo mwenye Miaka 24 hivi sasa anapimwa afya kabla kusaini Mkataba wa Miaka Mitano
Van Dijk alijiunga na Celtic Mawaka 2013 akitokea Groningen wa huko kwao.
Alex Song, Victor Moses & Nikica Jelavic wasaini West Ham
West Ham wamemsaini Kiungo wa Barcelona Alex Song na pia Winga wa Chelsea anaetoka Nigeria Victor Moses kwa Mkopo wa Msimu mmoja huku Straika wa Hull City Nikica Jelavic akitua kwa Dau la Pauni Milioni 3.
Song, Mchezaji wa Cameroun mwenye Miaka 27, aliichezea West Ham Mechi 31 Msimu uliopita akiwa hapo kwa Mkopo kutoka Barcelona ambako aliuzwa na Arsenal Mwaka 2012.
Moses, mwenye Miaka 24, hii Leo alisaini Mkataba mpya wa Miaka Minne na Klabu yake Chelsea lakini amepelekwa kwa Mkopo West Ham na hii ni Klabu yake ya Tatu kuichezea kwa Mkopo tangu ajiunge na Chelsea Mwaka 2012 na kupelekwa kuzichezea Liverpool na Stoke City.
Nae Jelavic, Raia wa Croatia mwenye Miaka 30, anatarajiwa kusaini Mkataba wa Miaka Miwili na West Ham ambayo Meneja wao mpya ni Slaven Bilic aliekuwa Kocha wa Timu ya Taifa ya Croatia.
Regan Poole: Man United kumnunua toka Newport
Manchester United wametoa Ofay a Pauni 100,000 kumnunua Kinda wa Miaka 17 anaechezea Newport County, Beki Regan Poole, ambae Dili yake huenda ikapanda na kufikia Pauni 400,000.
Hivi sasa Kijana huyu yuko huko Man United akipimwa afya yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni