UPDATES MPYA : YAKIWA YAMEBAKI MASAA MAWILI HIZI NDIZO HABARI MPYA ZA USAJILI
Kama hujui ni kwamba hadi sasa pesa kiasi cha pound 813,750,000 zimetukika kwenye usajili wa kipindi hiki. Hizi hapa ndio habari moya kwenye usajili unaendelea kwa kasi hivi sasa.
Islam Feruz leo amejiungana na Hibernian kwa mkopo akitokea Chelsea hadi mwisho wa msimu huu.
Tottenham na Emmanuel Adebayor wapo kwenye mazungumzo ya kuvunja mkataba wake. Adebayo ambae ana miaka 31 lakini akiwa sio kwa kuwa free agent ambapo anategemewa kuwa hivyo baada ya kuvunja mkataba na Spurs.
Mwandishi Sami Mokbel anasea Arsenal hawategemei kufanya biashara yoyote nyingine zaidi ya kutaka kumsajili Cavani ambapo usajili huo bado unaenda kwa taratibu sana licha muda kuwa tupa mkono.
Chelsea wamekamilisha usajili wa mchezaji wa Senegal Nantes’ Papy Djilobodji.
Javier Hernandez amesema kwamba amejiunga na Leverkusen kwasababu ya mapenzi waliyomuonyesha. Anasema kwamba haikua ngumu kwake kujiunga na Leverkusen kwasababu alijiskia kwamba wanamuhitaji.
Ripota mwingine amesema kwamba Cavani kusajiliwa na Arsenal inakua ni vigumu kwasababu PSG wanahitaji £50m lakini Arsenal wanakua wagumu kuzitoa hizo pesa.
Aston Villa wametoa ripoti ya kukamilisha usajili wa Joleon Lescott kutoka West Brom kwa gharama ya £2m.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni