VIOJA MWISHONI UHAMISHO: SPURS, CHELSEA, MAN UNITED ZAAMBIWA TOENI £70M KUMNUNUA STAA WA BELGIUM!
Dirisha la Uhamisho huko England litafungwa Jumanne Septemba Mosi Saa 2 Usiku kwa Saa za Bongo.
Kiungo huyo Mbelgiji mwenye Miaka 26 anawindwa na Klabu kadhaa huko Ulaya na Zenit wameamua kuzuia hilo au kukamua sana ikibidi aondoke kwa kuweka Dau la juu mno.
Licha ya Mchezaji mwenyewe kuonyesha nia ya kutaka kuhama baada ya kutoboa kuwa alishaongea na AC Milan ya Italy na Klabu moja ya Ligi Kuu England ambayo hakuitaja, Zenit imegoma katakata kumruhusu aondoke.
Meneja wa Zenit, Andre Vilas-Boas, ambae aliwahi kuwa Chelsea na Tottenham, amekuwa akiongea na Staa huyo wa Belgium ili asihame na sasa uongozi wa juu umeingilia kati na kubandika Dau la kukimbiza Klabu nyingine.
TASS, Shirika la Habari la Urusi, limekariri Viongozi wa Zenit wakidai Witsel ana Kipengele cha Mkataba wake kinachotaka walipwe Pauni Milioni 70 ikiwa atataka ahame kabla ya Mkataba wake kwisha na bila ya ridhaa yao
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni