WACHEZAJI WA CHELSEA WAINGIWA NA HOFU
Chelsea tayari imekwisha poteza
michezo mitatu katika mechi tano za awali huku ikielezwa kuwa hali ya
wasiwasi miongoni mwa wachezaji ikiwa ni kubwa zaidi.
Kocha Jose Mourinho hataki
kupaniki na wala hajaitisha mkutano wowote wa ‘crisis’ kuelekea katika
mchezo wa klabu bingwa Ulaya dhidi ya Maccabi Tel Aviv katika uwanja wa
Stamford Bridge.
Chelsea imevuna points nne pekee
katika katika michezo mitano ya ligi msimu huu, ikizidiwa points 11 na
viongozi wa ligi Manchester City wenye points 15, kitu kinachowapa hofu
wachezaji wa Chelsea namna gani ni vigumu kuziba pengo hilo.
Inaelezwa kuwa hali ya morali ya
timu iko chini sana katika kikosi hicho, huku ukiwa ni mwanzo mbaya
zaidi katika historia ya klabu tangu mwaka 1988.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni