MKONGWE WA ARSENAL ATAJA MBADALA WA WENGER
Baada ya mashabiki wa Arsenal
kulalamika sana kuhusu kocha wao na watu mbalimbali bado wanajaribu
kutoa maoni yao nani anaweza kuwa kocha mpya.Robert
Pires ametoa maoni yake juu ya nani anadhani angeweza kutwaa mikoba ya
Arsene Wenger, na kusema kuwa ama Carlo Ancelotti au Thierry Henry ndio
wanastahili kiti hicho japokuwa asingependa kuona Mfaransa huyo
anaondoka hivi karibuni.
Wenger amekuwa katika msukumo
mkubwa katika miezi ya hivi karibuni kutoka mashabiki wa Arsenal, ambao
wanataka mafanikio ya haraka kwa timu yao, lakini Pires alipoulizwa
alijibu, “Nani ni mbadala sahihi? Thierry Henry? ndio, analijua soka
vizuri pamoja na Arsenal. Sijui…lakini nampenda zaidi Carlo Ancelotti”.
Lakini hata hivyo, Pires amegoma
kusema kuwa kocha wake huyo wa zamani wakati wake umekwisha, kwa haraka
alijibu hivi, “Lakini hayo ni maoni yangu tu, haina maana kwamba Arsenal
inamhitaji Ancelotti kwa wakati huu. Wenger bado ana mkataba na
Arsenal”.
Katika sehemu ambayo Wenger amekuwa akilaumiwa sana ni suala la usajili ili kukiboresha kikosi chake.
Lakini Pires analichukulia suala
hilo kwa utofauti kidogo, na kusema, “Nisingependa kusema kuwa Arsenal
wamefanya kosa lolote katika suala la usajili. Kama unaichezea Arsenal,
maana yake ni kwamba una ubora fulani. Miongoni mwao ni wachezaji
wakubwa sana ulimwenguni.
“Kwa upande wangu, usajili bora
kabisa wa Arsenal ni Santi Cazorla. Mashabiki wanampenda Alexis Sanchez,
je, vipi kwa upande wangu; Amekuwa ni mwepesi wa kuendana na mazingira
ya ligi mpya ya EPL-lakini Cazorla ni mtu muhimu sana. Kwa miezi
michache iliyopita , amekuwa ni mchezaji wetu bora”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni