ARSENAL ‘TEJA’ KWA CHELSEA, YATWANGWA KWAO EMIRATES, DIEGO COST ‘KILA!’
LIGI KUU ENGLANDMatokeo:
Jumapili 24 Januari 2016
Everton 1 Swansea 2
Arsenal 0 Chelsea 1
++++++++++++++++++++
Kipigo hiki cha 1-0 cha Chelsea kwa Arsenal ni muendelezo wa vipigo mfululizo kuanzia 2010 lakini Leo ndio cha kuuma sana kwani kimewatupa Arsenal Nafasi ya 3 kwenye Ligi Kuu England wakiwa nyuma ya Vinara Leicester City na Man City.
Arsenal, wakiwa kwao Emirates, walipata balaa Dakika ya 18 tu baada ya Sentahafu wao, Per Mertesacker, kumwangusha Diego Costa aliekuwa akichanja mbuga kumuona Kipa na Refa Mark Clattenburg kuamua ni Kadi Nyekundu ingawa tukio hili limegawa pande kila Mtu akibaki na nini alichoona yeye.
Upungufu huo ulimfanya Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amtoe Straika Olivier Giroud, na kumwingiza Sentahafu Mbrazil Gabriel Paulista ambae ndie alitoa uchochoro Dakika 5 baadae kwa Diego Costa kufunga Bao pekee na la ushindi.
VIKOSI:
Arsenal: Cech; Bellerín, Koscielny, Mertesacker, Monreal; Flamini, Ramsey; Campbell, Özil, Walcott; Giroud
Akiba: Ospina, Chambers, Gibbs, Gabriel, Elneny, Oxlade-Chamberlain, Sánchez.
Chelsea: Courtois; Ivanovic, Zouma, Terry, Azpilicueta; Mikel, Matic; Willian, Fàbregas, Oscar; Costa
Akiba: Begovic, Cahill, Baba Rahman, Loftus-Cheek, Traore, Hazard, Rémy.
REFA: Mark Clattenburg
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
Jumanne 2 Februari 2016
[Mechi kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku]
Arsenal v Southampton
Leicester v Liverpool
Norwich v Tottenham
Sunderland v Man City
West Ham v Aston Villa
[Mechi kuanza Saa 5 Usiku]
Crystal Palace v Bournemouth
Man United v Stoke
West Brom v Swansea
Jumatano 3 Februari 2016
[Mechi kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku]
Everton v Newcastle
Watford v Chelsea
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni