BARCELONA YAPATA POINTI 3 MESSI KAMA KAWA NYAVUNI
Jana ligi ya Hispania maarufu kama La Liga iliendelea kwa michezo minne, Barcelona wakiwa ugenini walipata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Malaga na kukusanya pointi tatu muhimu.
Munir aliindikia Barcelona bao la kwanza lakini lilisawazishwa na Juanpi dakika ya 32.
Lionel Messi akaibeba Barcelona kwa kuifungia bao la ushindi dakika ya 52. Barcelona jana iliwakosa nyota wake muhimu kwenye ushindi huo, Neymar na Gerrard Pique waliukosa mchezo huo.
Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa jana yako hivi:
Espsnyol 2-2 Villarreal
Granada3-2 Getafe
Rayol Vallecano 3-0 Celta Vigo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni