tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

25 Januari 2016

HATMA YA VAN GAAL MAN UTD KUJULIKANA WAKATI WOWOTE

Van Gaal 2
Kibarua cha kocha Louis Van Gaal wa Manchester United sasa kipo katika hatua mbaya zaidi hivi sasa kutokana na taarifa kuwa tayari makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Ed Woodward kukutana na wachezaji wakubwa wa klabu hiyo kutaka kujua nini kinaleta shida hata kusababisha timu hiyo kutokua na matokeo mazuri msimu huu.
Ed Woodward anajua hali iliyopo sasa kwa wachezaji wa Manchester United wamechoka kuzishikilia mbinu za kocha Louis Van Gaal na hawajitolei kwa asilimia 100.
Baadhi ya watu wamemshauri msaidizi wa kocha huyo Ryan Giggs kujiondoa wadhifa wake ili kuongeza presha kwa kocha Louis Van Gaal afutwe kazi klabuni hapo.
Habari zinasema kuwa huenda Ryan Giggs akapewa mikoba hiyo tofauti na taarifa zinazotoka katika kambi ya aliyekua kocha wa Chelsea Jose Mourinho ambazo zinaeleza nia ya Mourinho kuwa na njaa ya kukinoa kikosi cha mashetani wekundu.
Kipigo cha bao 1-0 nyumbani Old Trafford weekend hii toka kwa Southampton kimeongeza presha kwa kocha Louis Van Gaal baada ya kuwa points 5 nyuma ya timu inayoshika nafasi ya nne Tottenham Hotspur.

Hakuna maoni: