Jay Z anaifukuzia saini ya Marcus Rashford wa Man United
Kampuni ya uwakala wa wanamichezo ya mwanamuziki huyo, Roc Nation Sports, ni moja ya taasisi/watu wanaowania saini ya kumuwakilisha kinda huyo wa Manchester United.
Mawakala wenye majina makubwa kwenyebsoka wamekuwa wakipigana vikumbo kumsaini Rashford mwenye umri wa miaka 18, ambaye kwa sasa anawakilishwa na familia yake.
Familia yake inategemewa kuendelea kudili na madili ya mtoto wao lakini hilo halijawafanya mawakala wengine kujaribu kutaka kufanya kazi na Rashford, huku Roc Nation ikijaribu kutaka kuanza makubaliano na familia ya kinda huyo wa kiingereza.
United wanategemewa kumpa Rashford mkataba mpya mwishoni mwa smimu baada ya kuonyesha kiwango bora msimu huu tangu alipopewa nafasi katika kikosi cha kwanza.
Rashford amebakiwa na mwaka mmoja katika mkataba wake wa zamani na sasa anategemea kupata mkataba ambao atakuwa akiingiza angalau £15,000 kwa wiki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni