tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

16 Aprili 2016

LA LIGA: LEO REAL UGENINI NA GETAFE, ZIDANE AMPIGIA DEBE RONALDO KUZIDI KUFUNGA!

RONALDO-AIMALIZA-WOLFSBURGKOCHA wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema hamna sababu ya kuwa na wasiwasi na Cristiano Ronaldo kuhusu uchezaji wake kwani Siku zote hufunga Magoli.
Juzi, Kati-Wiki, Ronaldo aliibomoa Wolfsburg ya Germany kwa kupiga Bao 3 wakati Real LALIGA-APR15inashinda 3-0 na kutinga Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambako watakutana na Man City.
Kuna Wachambuzi huko Spain wamedai Ronaldo, mwenye Miaka 31, ameporomoka Kisoka lakini Supastaa huyo amepiga Bao 5 katika Mechi za Real za Mwezi huu.
Pia Ronaldo alipiga Bao la ushindi wakati Real inaifunga Barcelona kwenye El Clasico huko Nouu Camp.
Na Zidane amesisitiza: “Hilo hutokea lakini Ronaldo Siku zote atafunga Magoli. Cristiano atacheza Mechi na Getafe!”
Ronaldo ndie anaongoza kwa Ufungaji Bora wa La Liga Msimu huu akiwa na Magoli 30 na hiyo ni Rekodi ya kuwa Mtu wa Kwanza katika Historia ya La Liga kupiga Bao 30 au zaidi kwa Misimu 6 mfululizo.
LALIGA-TS-APR15Real wapo Nafasi ya 3 kwenye La Liga wakiwa Pointi 4 nyuma ya Barcelona ambao wameporomoka hivi karibuni kwa kupoteza Mechi mfululizo.
Zidane ameeleza: “Sisi hatuwezi kufanya lolote kuhusu Barcelona. Mkazo ni kitu gani tunafanya sisi.”
Leo Real wako Ugenini kucheza na Getafe na ushindi kwao utawaweka Pointi 1 nyuma ya Barcelona ambao wanacheza Jumapili na Valencia.
Timu ya Pili Atletico Madrid, ambao wako Pointi 1 mbele ya Real, Leo wanacheza na Granada.
LA LIGA
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
Ijumaa Aprili 15
Levante 2 RCD Espanyol 1           
Jumamosi Aprili 16
1700 Getafe CF v Real Madrid CF
1915 Las Palmas v Sporting Gijon
2130 SD Eibar v Real Sociedad
2305 Celta de Vigo v Real Betis
Jumapili Aprili 17
1300 Malaga CF v Athletic de Bilbao
1700 Sevilla v Deportivo La Coruna
1915 Atletico de Madrid v Granada
1915 Rayo Vallecano v Villareal
2130 FC Barcelona v Valencia

Hakuna maoni: