Picha; Wakati dili la Mourinho likionekana kufa, Ferguson aonekana kwenye mkutano wa siri na Pochettino
Wakati mashabiki wengi wa Manchester United wakiwa na hasira na
hofu baada ya leo asubuhi kushuhudia mchezaji ambaye alikuwa
akihusishwa na kujiunga na Man United kwa muda mrefu Renato Sanchez
akijiunga na Bayern Munich, jambo lilopelekea uvumi wa kocha Jose
Mourinho kujiunga na United kuingia shakani, jioni ya leo kocha wa
zamani wa United na mjumbe wa bodi Sir Alex Ferguson leo jioni
ameonekana akitoka kwenye kikao cha siri na kocha wa Tottenham Hotspur,
Mauricio Pachettino.

Ferguson na Pochettino walionekana wakitoka kwenye kikao chao jioni ya leo katika mgahawa wa Mayfair.
Pochettino ni mmoja wa makocha ambao wanapewa nafasi ya kumrithi
Louis van Gaal pale Old Trafford mwishoni mwa msimu huu pamoja na kwamba
tayari amekubaliana kimsingi na Spurs kuendelea nao mpaka 2021.

Kocha
huyo wa zamani Southampton aliukosa ubingwa wa EPL ulioenda mikononi
mwa Leicester na kuiongoza kwake vizuri Spurs kumewavutia maboss wa
United na namna alivyoweza kuwaongoza vijana wadogo akiwemo mchezaji
bora chipukizi Dele Alli.

Hata
hivyo, Jose Mourinho bado anabaki kocha anayepewa nafasi ya kumrithi
Van Gaal pale Theatre of Dreams baada ya kunyimwa kazi mwaka 2013.
Kocha msaidizi wa United Ryan Giggs na kocha wa Paria Saint Germain
Laurent Blanc wamekuwa wakitajwa kuweza kurithi hiyo nafasi, ingawa kuna
uwezekano mkubwa sasa kwamba huenda Van Gaal ataruhusiwa kuendelea na
msimu mmoja mwingine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni