tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

9 Juni 2016

FIFA YAIOSHA CHELSEA KUHUSU MOHAMED SALAH KUCHEZA AS ROMA!

SALAHJANA FIFA imetoa tamko kuwa Uhamisho wa Mkopo wa Mohamed Salah kutoka Chelsea kwenda AS Roma haukubunja Mkataba wowote.
Uamuzi huo umetupa nje malalamiko ya Klabu ya Serie A ya Italy Fiorentina ambao walidai Chelsea walivunja Mkataba na wao kwa kumtoa kwao kwa Mkopo na kumpeleka AS Roma kwa Mkopo pia Msimu uliopita.
Salah, Mchezaji wa Kimataifa wa Egypt, alihamia Chelsea kutoka FC Basel Januari 2014 na Mwaka mmoja baadae akaenda Fiorentina kwa Mkopo na kuichezea Mechi 16.
Msimu uliofuata, yaani Msimu uliopita, Salah, mwenye Miaka 23, akaondoka Fiorentina na kuhamia AS Roma kwa Mkopo na hapo ndipo Fiorentina wakaja juu wakidai walipewa haki ya kumbakiza na pia kumnunua moja kwa moja.
Jana FIFA ilithibitisha kwamba suala hilo lilikuwa kwao DRC, Dispute Resolution Chamber, Chemba ya Kutatua Migogoro na kwamba madai ya Fiorentina yamekataliwa.
Salah bado ni Mchezaji wa Chelsea na upo uwezekano Msimu ujao akarudi Stamford Bridge kucheza chini ya Meneja Mpya Antonio Conte.

Hakuna maoni: