tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

9 Juni 2016

MARADONA ANASWA ‘AKIMTUMBUA’ MESSI MBELE YA PELE!

MARADONA-MESSILEJENDARI wa Argentina Diego Maradona amenaswa akimteta Muargentina mwenzake Lionel Messi wakati akiongea na Lejendari wa Brazil Pele huko Paris hii Leo.PELE-MARADONA
Katika mazungumzo hayo ambayo yalirekodiwa bila Maradona kujijua yuko kwenye Kinasa Sauti, alisikika akisema Lionel Messi, ambae sasa ndie Kepteni wa Timu ya Taifa ya Argentina, hana uthabiti wa kuwa kiongozi.
Wakiwa pamoja, wakiamini wanazungumza wao tu bila kurekodiwa, Pele alimuuliza Maradona kama anamjua binafsi Messi.
Maradona alijibu: “Yeye ni Mtu mzuri sana lakini hana mvuto. Anakosa uthabiti wa kuwa kiongozi.”
Pele akajibu: “Ah, nakupata, yeye si kama sisi enzi zetu. Katika Miaka ya 1970, Brazil ilikuwa na Wachezaji wazuri sana kama Rivellino, Gerson, Tostao. Si kama Argentina ya sasa ambayo inamtegemea Messi tu. Maradona anasema Messi ni Mchezaji mzuri, bila shaka, lakini hana mvuto!”
Maneno haya ya Maradona kwa muda mrefu yanafanana na imani ya Waargentina wengi ambao wamekuwa wakivunjwa moyo na kujituma kwa Messi akiwa na Timu ya Taifa ya Argentina tofauti na akiwa na Klabu yake Barcelona.
Messi, mwenye Miaka 28, akiwa na Argentina mara 2 amepoteza Fainali za Copa America na mara moja ile ya Kombe la Dunia, akibaki amevuna tu Medali ya Dhahabu ya Olimpiki Mwaka 2008 Argentina iliposhinda Michezo ya Olimpiki ya Mwaka huo.
Jana, Messi alikuwa Benchi wakati Argentina ikicheza Mechi yao ya ufunguzi ya Kundi lao la Mashindano ya Copa America huko USA walipowafunga Mabingwa Watetezi Chile 2-1.

Hakuna maoni: