tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

20 Agosti 2016

Manchester United 2-0 Southampton



Manchester United 2-0 Southampton

    Manchester United imepata ushindi wake wa pili kwenye ligi kuu ya Uingereza baada ya kuilaza Southampton mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa kweny dimba la Old Trafford Ijumaa usiku.

    Zlatan Ibrahimovic ameifungia Man Utd mabao yote mawili, la kwanza akifunga kwa kichwa kutoka krosi ya Wayne Rooney kwenye dakika ya 36 kipindi cha kwanza huku bao la pili akifunga kipindi cha pili dakika ya 53.

    Alifunga kwa mkwaju wa penati baada ya Luke Shaw kuangushwa kwenye eneo la hatari.



    Shauku kubwa ya mashabiki wa Manchester United ilikuwa kumuona mchezaji ghali zaidi duniani, Paul Pogba akiitumikia Manchester United kwa mara ya pili.

    Mourinho alimpanga Pogba katika kikosi chake kilichoanza, alifanya mabadiliko ya mchezaji mmoja tu kwa kikosi kilichoanza dhidi ya Bournemouth ambapo Herrera alimpisha Pogba.

    Kiungo huyo wa Kimataifa wa Ufaransa ameonyesha ubora wake na amedhihirisha kuwa atakuwa nguzo muhimu kwa Manchester United msimu huu.

    Katika mchezo huo amecheza dakika zote tisini, hakuwaangusha mashabiki wa Manchester United.

    Erick Bailly mlinzi wa kati wa Manchester United pia alikuwa kikwazo kwa vijana wa Southampton waliotwala mchezo huo kwenye kipindi cha kwanza.

Hakuna maoni: