GUARDIOLA AMWAMBIA JOE HART NENDA UKITAKA!
Tangu atue Guardiola hapi City, Hart amepigwa Benchi na namba yake kuchukuliwa na Kipa kutoka Argentina Willy Caballero ambae amedaka Mechi zote 2 za Masimu mpya.
Caballero alicheza wakati City inaifunga Sunderland kwenye Mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England, EPL, Wikiendi iliyokwisha na pia kudaka Alhamisi Usiku wakati City inaitandika Steau Bucharest 5-0 huko Romania kwenye Mechi ya kwanza ya Raundi ya Mwisho ya Mchujo ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Inasemekana Hart, mwenye Miaka 29 na Kipa Namba Wani wa England,
anatafakari kuondoka City acheze kwa mkopo kwingine na Guardiola amesema: “Sitaki Wachezaji wabaki kama hawataki. Wakitaki kubaki wabaki na kupigania namba.”
Hivi sasa kuna minong’ono City ipo mbioni kumnasa Kipa na Makipa wa Barcelona Claudio Bravo na Marc-Andre ter Stegen wanatajwa.
LIGI KUU ENGLAND
Msimu Mpya 2016/17Ratiba:
**Saa za Bongo
Ijumaa Agosti 19
2200 Man United v Southampton
Jumamosi Agosti 20
1430 Stoke City v Man City
1700 Burnley v Liverpool
1700 Swansea v Hull
1700 Tottenham v Crystal Palace
1700 Watford v Chelsea
1700 West Brom v Everton
1930 Leicester City v Arsenal
Jumapili Agosti 21
1530 Sunderland v Middlesbrough
1800 West Ham v Bournemouth
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni