tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

24 Machi 2017

24 March 2017 habari kubwa magazeti Ulaya.


Daily Express. Gazeti hili limetoa taarifa kihusiana na Mitchy Batshuayi ambae wakala wake ameshindwa kukataa fununu zinazosema kwamba Mfaransa huyo ataihama klabu hiyo mwisho wa msimu huu. Granit Xhaka amejitetea kuhusu rafu zake anazocheza msimu huu kwa kudai kuwa huwa hakusudii kumuumiza mtu au kucheza vibaya.

Daily Mail. Gazeti la Daily Mail limesema Liverpool wamezidisha kasi katika mbio za kumsajili beki wa Burnley Michael Keane baada ya kiwango bora alichoonesha dhidi ya Ujerumani. Beki wa kushoto wa Schalke 04 Sead Kolasinic anaweza kujiunga na Man City mwishoni mwa msimu huu.

The Sun. Antoine Griezman bado tu anahusishwa na kujiunga na Man United katika deal 
litakalowacost United kiasi cha £86m. Man City wanajiandaa kutuma dau la £40m kwa Juventus ili kumchukua winga Kingsley Coman aliyeko Bayern Munich kwa mkopo. Mashabiki wa Arsenal wanajipanga kujichangisha £904m ili kuinunua timu yao kutoka kwa mmiliki wake baada ya kuona anawazingua.

Daily Mirror. Tottenham wako tayari kumuachia Moussa Sissoko aondoke baada ya kudumu klabuni hapo kwa msimu mmoja. Wakati Arsenal na Liverpool wakipigana vikumbo kumpata kiungo wa Schalke Leon Goretzka, Man United na Liverpool nao wanapigana vikumbo kumchukua Jose Gimenez kutoka Atletico Madrid.
The Guardian nalo linasema Real Madrid wanaweza kuibomoa Chelsea msimu huu kwa kuchukua wachezaji wao wawili muhimu golikipa Thibaut Courtois na Eden Hazard.

Hakuna maoni: