SPURS RUKSA WEMBLEY MECHI ZA NYUMBANI MSIMU UJAO!
KUPISHA KITU KIPYA WHITE HART LANE!
Brent Council, Halmashauri ambayo Uwanja huo upo, imepitisha kwa Kura uamuzi wa kuiruhusu Spurs kutumia Wembley kwa Mechi zao 27 na kuruhusu Uwanja wote kujazwa Watu 90,000.
Spurs wamepewa hadi Machi 31 kuthibitisha matumizi hayo.
Hivi sasa Spurs wanajenga Uwanja wao mpya jirani na ule wa sasa White Hart Lane na ambao unatarajiwa kuwa tayari kutumika kwenye Msimu wa 2018/19.
Sasa Spurs wanatafakari kama waendelee kuutumia White Hart Lane kwa Msimu ujao na ule wa 2018/19 ili wahamie Uwanja Mpya Msimu wa 2019/20.
Spurs hawakutaka kuutumia Wembley huku wakiwekewa sharti la Uwanja kutojazwa na Halmashauri ya Brent ambayo baadhi ya Wajumbe wake walipinga Uwanja kujazwa wote kutokana na kuogopa vitendo vya kihuni vya Washabiki na pia kuzorotesha Usafiri wa Eneo lao.
Wajumbe hao walitaka Spurs waruhusiwe kutumia Wembley kwa ujazo wa Watu 61,000 tu na si 90,000 kama vile uwezo wa Wembley yenyewe.
Kukubaliwa kwa Spurs kucheza Mechi 27 tu kuna sharti kuwa Mechi zikizidishwa zaidi ya hapo basi hawataruhusiwa kuwa na Washabiki zaidi ya 50,835 kwa Mechi za ziada.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni