tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

24 Machi 2017

DELE ALLI ‘JELA’ MECHI 3 ULAYA!


UEFA YAZIPIGA FAINI ARSENAL, BAYERN NA ST-ETIENNE!
DELE-ALLI-JINAKIUNGO wa Tottenham Dele Alli amefungiwa Mechi 3 za Ulaya baada ya kutolewa kwa Kadi Nyekundu Timu yake ilipocheza na KAA Gent ya Belgium Uwanjani Wembley Mwezi Februari kwenye Mechi ya UEFA EUROPA LIGI.
Alli alitolewa alipomvaa Mchezaji wa Gent Brecht Dejaegere kwenye Droo ya 2-2 na sasa UEFA imdethibitisha Adhabu yake.
Ikiwa Spurs watafuzu ndani ya 3 Bora ya EPL, Ligi Kuu England, basi Alli hatacheza Mechi 3 za Makundi ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, Msimu ujao na hizo ni Nusu za Mechi za Awamu hiyo.
Wakati huo huo, Arsenal nayo imepigwa Faini ya Pauni 4,300 na UEFA kwa kosa la Mashabiki wao kuvamia Uwanja wa Kuchezea walipodundwa 5-1 na Bayern Munich Uwanjani Emirates.
UEFA pia imeipiga Faini Bayern Munich ya Pauni 2,600 baada ya Mashabiki wao kusababisha Mechi hiyo na Arsenal kuchelewa kuanza waliporusha Uwanjani Mabunda ya Karatasi za Chooni wakilalamikia Bei ya Juu ya Tiketi za Viingilio.
Timu nyingine iliyopigwa Faini na UEFA ni Saint-Etienne ya France ambayo itapaswa kulipa Pauni 43,000 baada ya Mashabiki wao kufyatua Fataki za Moto Uwanjani Old Trafford Mwezi uliopita walipofungwa na Manchester United kwenye Mechi ya UEFA EUROPA LIGI.

Hakuna maoni: