ARSENAL NA WENGER: BODI KUKETI JUMANNE, NINI KITAZUKA?
Furaha hiyo haifichi ukweli kuwa Msimu huu Arsenal, kwa mara
nyingine tena, wamefeli na hasa kwa kumaliza Nafasi ya 5 kwenye EPL,
LIGI KUU ENGLAND, na kukosa kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao ikiwa
ni mara yao ya kwanza katika Miaka 20.
Sasa, Arsenal, kwa Nafasi yao ya Ligi, ambayo pia kubeba FA CUP inawapa, Msimu ujao watacheza UEFA EUROPA LIGI Hatua ya Makundi.
Wenger, mwenye Miaka 67, amewashambulia wapondaji wake na kuwaita
ni fedheha na hatawasahau kwani wamemvunjia heshima na kusahau mafanikio
yake katika Miaka 20 ya himaya yake hapo Arsenal.
Katika kipindi hicho, Wenger ameipa Arsenal FA CUP 7 na Ubingwa wa EPL mara 3.
Sasa maamuzi yote ya Wenger kubaki au kuondoka yataamuliwa na Bodi ya Arsenal Jumanne.
Laki swali kubwa ni Je Wenger asipopewa Mkataba Mpya wa kuendeleza huu wa sasa unaoisha Juni nani atakuwa Mrithi wake?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni