tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

30 Mei 2017

HANG’OKI NG’O: WENGER AKUBALI MKATABA MPYA MIAKA 2 ARSENAL!!


HABARI MPYA ZILIZOPASUA hivi punde toka huko London zimedai Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameafiki Mkataba Mpya wa Miaka Miwili wa kuendeleza himaya yake ya Miaka 21 Klabuni hapo.
Jana Wenger na Mmiliki wa Hisa nyingi za Arsenal, Stan Kroenke, walikutana ili kuamua hatima yake na kuachia uamuzi wa mwisho kufanywa na Bodi ya Arsenal iliyoketi Leo Jijini London.
Klabu ya Arsenal imedokeza itatoa tamko rasmi Jumatano.
Mkataba wa Wenger hivi sasa unaishi Mwezi Juni.
Msimu huu uliokwisha Majuzi, Arsenal ilimaliza Nafasi ya 5 kwenye EPL, LIGI KUU ENGLAND, na kukosa kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao ikiwa ni mara yao ya kwanza katika Miaka 20 tangu Wenger ajiunge Mwaka 1996.
Sasa, Arsenal, kwa Nafasi yao ya Ligi, ambayo pia kubeba FA CUP inawapa, Msimu ujao watacheza UEFA EUROPA LIGI Hatua ya Makundi.
+++++++++++++++
HABARI ZA AWALI:
ARSENAL NA WENGER: BODI KUKETI JUMANNE, NINI KITAZUKA?

WENGER-WINNER FACUP17JUZI Arsene Wenger alicheka sana na kuwavaa wapondaji wake baada ya Timu yake Arsenal kubeba FA CUP kwa kuwabwaga Mabingwa Wapya wa England Chelsea 2-1.
Furaha hiyo haifichi ukweli kuwa Msimu huu Arsenal, kwa mara nyingine tena, wamefeli na hasa kwa kumaliza Nafasi ya 5 kwenye EPL, LIGI KUU ENGLAND, na kukosa kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao ikiwa ni mara yao ya kwanza katika Miaka 20.
Sasa, Arsenal, kwa Nafasi yao ya Ligi, ambayo pia kubeba FA CUP inawapa, Msimu ujao watacheza UEFA EUROPA LIGI Hatua ya Makundi.
Wenger, mwenye Miaka 67, amewashambulia wapondaji wake na kuwaita ni fedheha na hatawasahau kwani wamemvunjia heshima na kusahau mafanikio yake katika Miaka 20 ya himaya yake hapo Arsenal.
Katika kipindi hicho, Wenger ameipa Arsenal FA CUP 7 na Ubingwa wa EPL mara 3.
Sasa maamuzi yote ya Wenger kubaki au kuondoka yataamuliwa na Bodi ya Arsenal Jumanne.
Laki swali kubwa ni Je Wenger asipopewa Mkataba Mpya wa kuendeleza huu wa sasa unaoisha Juni nani atakuwa Mrithi wake?

Hakuna maoni: