BORUSSIA DORTMUND YAMTUPIA VIRAGO KOCHA WAKE
KLABU ya Borussia Dortmund imemfukuza kocha wake, Thomas Tuchel.
Mwalimu
huyo mwenye umri wa miaka 43, aliyerithi mikoba ya Jurgen Klopp Uwanja
wa Signal Iduna Park, anafukuzwa akitoka kuiongoza timu hiyo kutwaa
Kombe la Ujerumani mwishoni mwa wiki iliyopita.
Lakini taarifa za kutofautiana kwake na bodi ya klabu ndiyo inamfikisha kwenye kufukuzwa.
Taarifa
ya Dortmund imesema: Mabingwa mara nane wa Ujerumani, Borussia Dortmund
awametengana na kocha Thomas Tuchel. Haya ni matokeo ya mazungumzo
baina ya Hans-Joachim Watzke (Mtendaji Mkuu), Michael Zorc (Mkurugenzi
wa Michezo), Thomas Tuchel na Mshauri wake, Olaf Meinking yaliyofanyika
Jumanne,".
Dortmund imemshukuru Thomas Tuchel na wasaidizi wake kwa mafanikio waliyoleta BVB na kuwatakia kila heri baada ya kuondoka.
Gazeti la Bild limeandika kwamba sakata la Tuchel kuondolewa linaweza kuigharimu Dortmund kiasi cha Pauni Milioni 2.5.
Baada
ya kuchukua nafasi ya kazi katika klabu hiyo ya Ligi Kuu Ujerumani
Julai mwaka 2015, Tuchel akafanikiwa kuwa mmoja wa makocha bora katika
historia ya Dortmund akipata wastani wa pointi zaidi ya mbili kwa kila
mechi ya Bundesliga.
Ameshinda
mechi 69 kati ya 107 akiwa kazini, akimaliza nafasi ya pili nyuma ya
Bayern Munich katika msimu wake wa kwanza na ya tatu msimu huu.
Jumamosi
aliiongoza timu hiyo kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Eintracht
Frankfurt, ingawa tayari kulikuwa kuna matatizo ya ndani kwa ndani baina
yake na uongozi.
Hakufurahia
kuuzwa kwa wachezaji kama Henrikh Mkhitaryan, Ilkay Gundogan na Mats
Hummels msimu uliopita na tangu hapo uhusiano wake na Hans-Joachim
Watzke ukaharibika kabisa.
Tuchel inadaiwa alikorofishana pia na Msaka vipaji mkuu, Sven Mislintat na kufanya uwezekano wake wa kubaki uzidi kuwa mdogo.
Dortmund
sasa inaingia sokoni kutafuta kocha mwingine atakayemrithi Tuchel, huku
Lucien Favre akipwea nafasi kubwa ya kuchukua kazi hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni