Leo tarehe 12 May yasemavyo magazeti ya Ulaya.
The Sun linasema Gareth Bale atakuwa fiti siku mbili kabla ya fainali ya mashindano ya Champions League lakini hana uhakika wa kucheza fainali hiyo, klabu ya Chelsea imetuma mascout kumuangalia mlinzi a Bournamouth Adam Smith ambaye wako na mpango wa kumnunua.
Daily Mirror.Klabu ya Manchester City imeonesha nia ya kutaka kubaki na Jesus Navas baada ya klabu hiyo kuamua kumpa mkataba mpya mchezaji huyo, huko Leicester nako pamoja na tishio la wachezaji wake wakubwa kuondoka kocha wa klabu ya Leicester City Craig Shakespare ameamua kukaa na wachezaji wake kujaribu kuwashawishi wasiondoke.
Daily Mail.Pamoja na Arsenal kutaka kuajiri meneja wa masuala ya usajili lakini imefahamika Arsene Wenger ndio atakuwa na sauti ya mwisho katika masuala ya usajili, kocha wa Chelsea Antonio Conte inasemekana ameshaanza kuiambia klabu hiyo kuhusu mkataba mpya na kutaka alipwe kutokana na kazi kubwa anayofanya.
The Times.Klabu ya Chelsea ina mpango wa kuwapa pesa ya nyongeza wachezaji wake kama wakibeba kombe la ligi kuu, imebainika kila mchezaji wa Chelsea atakula kiasi cha £5m kama wakifanikiwa kubeba kombe hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni