Juventus kuifaidisha Chelsea kifedha kama ikibeba ubingwa wa UEFA.
Mashabiki wa Chelsea katika mchezo huo wanaweza kuchagua upande wowote kuushabikia lakini kwa sababu za kibiashara inaonekana Chelsea wanaweza ishabikia Juventus katika fainali hiyo.
Chelsea watafaidika kibiashara endapo Juventus watafanikiwa kuifunga Real Madrid katika mchezo huo na kubeba kombe hilo kwani kuna kiasi cha pesa wataweka mfukoni.
Imebainika Chelsea watapokea kiasi cha £3.5m kutoka kwa Juventus ikiwa ni sehemu ya makubaliano kati ya timu hizo mbili wakati wanapeana winga Juan Cuadrado.
Juventus wamekuwa wakiilipa Chelsea kiasi cha £4.5 kila mwisho wa msimu huku kukiwa na makubaliano ya pesa ya ziada kwa kila kombe ambalo Juventus watachukua wakati Curdado akiwa katika timu yao.
Makubaliano hayo kuhusu pesa ya ziada yataigharimu Juventus msimu huu kiasi hicho cha £3.5m kutokana na Juventus kubeba kombe la ligi na kombe la Champions League.
Curdado isajiliwa na Chelsea kutoka Fiorentina kwa dau la £23.3m lakini akashindwa kuonesha kiwango kikubwa ndani ya klabu hiyo, baada ya michezo 15 tu Chelsea waliamua kumtoa kwa mkopo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni