tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

1 Mei 2017

Magazeti ya Ulaya yasemacho leo siku ya wafanyakazi.

Twitter
Daily Mirror.Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Kun Aguero anafanyiwa vipimo leo ili kujua kama atakosa mechi zote za msimu zilizobaki ama laa, wakati huo huo klabu ya Manchester United inajaribu kuwapiku Manchester City na Arsenal katika usajili wa mchezaji wa Fulham Ryan Ssegnon.
Daily Mail. Gazeti la Daily Mail limeripoti kwamba klabu ya Chelsea bado ndio klabu inayoongoza katika mbio za kumsaini kiungo wa Monaco Tiomue Bakayoko ambaye Manchester United pia wanamtaka, Liverpool wameamua kuweka £40m kama dau endapo mshambuliaji wao Daniel Sturridge ataamua kuondoka.
Daily Express.Gazeti hili la Daily Express limesema kocha wa Manchester United Jose Mourinho amepanga kutumia £80m kwa ajili ya kumnunua kiungo wa Psg Blaise Matuidi na kiungo wa Monaco Bernardo Silva ili kuimarisha safu yake ya kiungo.
The Sun.Klabu ya Atletico Madrid iko kwenye mpango wa kumfanya Antoine Griezman kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika klabu hiyo na kuongeza kiwango cha fedha za kumuuzia ili kujaribu kuizuia Manchester United kumnunua, Romelu Lukaku yuko kwenye mpango wa kumtosa Jose Mourinho anayemtaka na kujiunga na klabu yake ya zamani ya Chelsea.
The Sun hilohilo linasema James Rodriguez atajiunga na Manchester United endapo David De Gea atajiunga na Real Madrid, Pep Gurdiola anajaribu kumtumia Kelechi Iheanacho kuwapa Borussia Dortmund ili amnase Pierre Aubemayang na wakati huo huo Gurdiola amebadili mawazo kuhusu Yaya Toure kwani anataka kumpa dili jipya la mwaka mmoja.

Hakuna maoni: